Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt.Wilson Mahera Charles ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa kutoa taarifa kwa umma.
"Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha jana tarehe 8 Septemba, 2020 imeendelea na zoezi la kupitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa za wagombea ubunge zilizowasilishwa na wagombea kupitia kwa wasimamizi mbalimbali wa uchaguzi nchi nzima.Zinazofanana soma hapa.
Rufaa hizo zimewasilishwa chini ya kifungu cha 40 (6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, ambacho kinatoa fursa kwa wagombea wa ubunge kukata rufaa wanapokuwa hawajaridhika na uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi kutokana na pingamizi zilizowasilishwa.
Katika kikao hicho, tume imepitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 34 kama ifuatavyo; imekubali rufaa 13 na kuwarejesha wagombea katika orodha ya wagombea. Rufaa hizo ni kutoka kwenye majimbo ya Singida Magharibi,
Madaba, Ilemela, Namtumbo, Bagamoyo, Liwale, Tunduma, Bukene na Kigamboni."Imekataa rufaa saba za wagombea ambao hawakuteuliwa. Rufaaa hizo ni kutoka kwenye majimbo ya Singida Magharibi, Bahi, Handeni Vijijini, Madaba, Singida Mashariki, Ileje, Meatu na Bukene.
"Imekataa rufaa 14 za kupinga walioteuliwa. Rufaa hizo ni kutoka kwenye majimbo ya Mwanga, Mafinga, Ilala, Manonga, Igunga na Kisesa.
"Idadi hii inafanya jumla ya rufaa za wagombea ubunge zilizofanyiwa uamuzi na tume kufikia 89, hii inafuatia taarifa kwa umma iliyotolewa jana tarehe 8 Septemba, 2020, ambapo tume ilitangaza uamuzi wa rufaa 55. Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku. Wahusika wa rufaa watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa tume,"amefafanua Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dkt.Wilson Mahera Charles.
Tags
Siasa