BREAKING NEWS: NEC yamtangaza Dkt.John Pombe Joseph Magufuli kuwa ndiye Rais mteule wa Tanzania

 

Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Semistocles S. Kaijage usiku huu amesema, matokeo haya ni baada ya zoezi la kutangaza matokeo ya awali ya Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukakamilika kwa kwa asilimia 100 kutoka majimbo yote 264 ya Tanzania Bara na visiwani, anaripoti Mwandishi Diramakini.

LIVE: NEC IKIMTANGAZA RAIS MTEULE TANZANIA

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Dkt.John Pombe Magufuli wa CCM ni Mshindi wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupata kura 12,516,252 akifuatiwa na Tundu Lissu wa CHADEMA kwa kura 1,933,271.

"Tume inamtangaza Dkt.Magufuli kuwa Rais wa Tanzania amepata kura nyingi halali kuliko Wagombea wengine wote na tunamtangaza Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania,"ameeleza Mwenyekiti wa NEC.

Amebainisha kuwa, jumla ya watu 15,91950 walipiga kura hizo wakati waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 29,754,699.

Katika majumuisho hayo, Mwenyekiti wa NEC amesema, kura halali zilikuwa milioni 14,830,195 huku kura zilizokataliwa zikiwa 261,755. Kwa matokeo hayo, wagombea urais wa vyama vingine wamegawana kura zilizosalia.

Pia kwa matokeo haya Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amefanikiwa kutetea nafasi yake baada ya kushinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano ya Oktoba 25, mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news