Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu Namba 55(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Dkt. Mwinyi Talib Haji kuwa Mwanasheria Mkuu Zanzibar.
Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Mwinyi Talib Haji alikuwa Naibu Katibu Mkuu Katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Tags
Zanzibar