Viingilio pambano la Mwakinyo dhidi ya Muargentina vyatangazwa

“Nimehama nyumbani na kujichimbia huku Magoroto kwa lengo la kufanya vyema katika pambano hilo, kujifua zaidi ya raundi 12 ili kupata stamina ya kwenda sambamba na mpinzani wangu;

Hassan Mwakinyo ameyasema hayo akiwa katika mazoezi makali kwa ajili ya kujiandaa kumkabili bondia Jose Carlos Paz kutoka Argentina, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mwakinyo ameweka kambi eneo la Magoroto mjini Muheza mkoani Tanga kuelekea pambano la kutetea ubingwa wa mabara wa WBF na kuwania ubingwa mpya wa mabara wa IBA wa uzito wa super-welter.

Bondia huyo anajifua chini ya kocha, Hamis Mwakinyo pamoja na wasaidizi mbalimbali huku wakitumia video mbalimbali kumsoma Paz ambaye ana rekodi nzuri.
 
Katika hatua nyingine, waandaaji wa pambano hilo wamesema kuwa tiketi kwa ajili ya pambano hilo zitauzwa mtandaoni kupitia kampuni za Nilipe na Selcom.
Mwakinyo akijifua kuelekea pambano dhidi ya Muargentina Novemba 13, mwaka huu kwenye ukumbi wa Next Door Arena, Oysterbay.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jackson Group Sports, Kelvin Twissa amesema kuwa, viingilio kwa pambano hilo vitaanzia sh. 150,000 kwa eneo la kawaida na meza ya watu 10 itauzwa kwa sh. milioni 3 ambao watapata huduma mbalimbali zilizoandaliwa.

Twissa amesema kuwa, mbali ya Mwakinyo na Paz, pia siku hiyo kutakuwa na pambano makali ambapo bondia nyota wa kike, Zulfa Macho atazipiga na Alice Mbewe kutoka Zambia wakati Hussein Itaba atazichapa na Alex Kabangu katika uzito wa super-middle.

Siku iyo pia bondia nyota kutoka Kenya, Fatuma Zarika atazichapa na Patience Mastara wa Zimbawe katika uzito wa super bantam. Wakati huo huo mpinzani wa Mwakinyo, Paz ameamua kuwasili mapema Tanzania ili kuzoea hali ya hewa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news