πŸ”΄#LIVE​​​: SIMBA SC vs AL HILAL Simba Super Cup, matokeo ni 4-1

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes wameibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal kwenye mchezo wa Simba Super Cup leo, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Katika dimba la Benjamin Mkapa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, mashabiki wengi ikiwa ni pamoja na wale waliokuwa wamevaa jezi ya Klabu ya Yanga wameonekana kuwa na furaha muda wote katika kandanda hilo safi.

Ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Gomes ambaye amerithi mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye ametimkia Morocco katika Klabu ya FAR Rabat alishuhudia uwezo wa nyota wake ikiwa ni pamoja na Rarry Bwalya aliyeanza kupachika bao la kwanza dakika ya 39.

Bao hilo lilisawazishwa na Salim Mohamed wa Al Hilal baada ya mabeki wa Simba kufanya uzembe huku Beno Kakolanya akishindwa kuokoa mchomo wa kichwa dakika ya 45.

Kipindi cha pili Perfect Chikwende alipachika bao la pili dakika ya 72 baada ya kipa wa Al Hilal kutema shuti lililopigwa na Bernard Morrison ambaye aliingia kipindi cha pili.

Morrison aliweza kufunga mabao mawili ambapo bao la tatu likiwa ni la pili kwake alifunga dakika ya 86 na lile la pili kwake likiwa la nne kwa Simba alifunga dakika ya 89.
Kocha Gomes amesema kuwa wachezaji wake walipambana kusaka ushindi jambo ambalo limewafanya waweze kuibuka na ushindi huo.

"Wachezaji wamepambana kusaka ushindi na wamefanikiwa hivyo naona kwamba wanastahili pongezi kwa kile ambacho wamekifanya,"amesema.

Morrison aliye katika msimu wake wa kwanza Simba SC tangu asajiliwe kutoka kwa mahasimu, Yanga Agosti mwaka jana alifunga mabao hayo baada ya viungo wengine wa kigeni, Mzambia Larry Bwalya na Mzimbabwe Perfect Chikwende kutangulia kufunga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news