Ofisi ya Rais TAMISEMI,inapenda kuwatangazia Umma kuwa,imekamilisha mchakato wa kuchambua maombi ya ajira ya Elimu na Afya iliyotangazwa tarehe 09/05/2021
Kuona Orodha ya Walimu Bofya hapa posted-applicants - 2021-06-25.pdf
Kuona Orodha ya Kada ya Afya Bofya hapa ORODHA YA WATUMISHI WA AJIRA MPYA KADA YA AFYA 25 JUNI, 2021.pdf
Akitoa taarifa hiyo jijini Dodoma, Prof. Shemdoe amesema waombaji wa kada ya Ualimu walikuwa 99,583 na Wataalam 37,437 wa kada ya afya, wakiwemo wenye ulemavu 1,099 waliomba nafasi hizo.Orodha ya majina yote soma hapa, bonyeza.
“Baada ya kukamilisha taratibu zote za uchakataji wa maombi Walimu 6,949 (3,949 wa shule za Msingi na 3000 wa shule za sekondari) na Wataalam wa kada za afya 2,726 wamepangiwa vituo vya kazi,” amesema Prof. Shemdoe
Ametaja vigezo vilivyotumika kuwapata watumishi waliokidhi sifa kuwa ni pamoja na Mwaka wa kuhitimu chuo ambapo waombaji waliomaliza mapema zaidi (mwaka 2012 hadi 2019) kulingana na mahitaji yaliyopo katika kada husika wamepewa kipaumbele.
Aidha, Umri wa mwombaji umezingatiwa kwa kutoa kipaumbele kwa waombaji wenye miaka zaidi ya 40 ambao wamemaliza miaka ya mwanzoni kama ilivyobainishwa kwenye kipaumbele cha awali.
“Sababu ni kuwa kama hawataajiriwa mapema wakifikisha miaka 45 ambapo hawataweza kuajiriwa tena Serikalini kwa ajira ya masharti ya kudumu” amesema Prof. Shemdoe.
Pia waombaji waliofungana kwa sifa zilizobainishwa awali yaani mwaka wa kuhitimu na umri amepewa kipaumbele msichana/mwanamke, bila kuathiri uwiano wa asilimia 50 amefafanua.Endelea kusoma hapa, bonyeza.
Tags
Tangazo