Kiongozi wa mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021 Luteni Josephine Paul Mwambashi akikabidhi Mwenge Maalum wa Uhuru kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Samia Suluhu Hassan, baada ya kufikia kilele cha mbio za Mwenge huo Maalum kwa Mwaka 2021 leo Oktoba 14,2021 katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti Kiongozi wa mbio za mwenge Maalum wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021 Luteni Josephine Paul Mwambashi kwa kutambua mchango wake mkubwa baada ya kuongoza kukimbiza Mwenge huo katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani, wakati wa maadhimisho ya kilele cha Mwenge huo yaliyofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita. (PICHA NA IKULU).
Tags
Picha