KALIUA,Vikundi 209 vya akinamama,
vijana na walemavu wanaojishughulisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo
kumiliki viwanda vidogo wilayani Kaliua mkoani Tabora wamewezeshwa kiasi cha sh.bililioni 1.184 ili kuboresha shughuli zao.
Hayo yamebainishwana Mkuu wa wilaya hiyo, Abel Busalama alipokuwa akielezea shughuli zilizofanywa
na halmashauri hiyo katika utekelezaji Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) katika kipindi cha Julai 2015 hadi Desemba 2019.
Alifafanua kuwa, mikopo
hiyo ni sehemu ya utekelezaji agizo la Serikali kwa kila halmashauri kutenga asilimia
10 ya mapato yake ya ndani ili kuwezesha wananchi kiuchumi, agizo hilo limetekelezwa
na halmashauri hiyo kwa uaminifu mkubwa.
Alibainisha kuwa, katika
kipindi hicho vikundi 122 vya akinamama vimekopeshwa jumla ya sh.milioni 492.95,
vikundi 78 vya vijana sh.milioni 326.8 na vikundi tisa vya walemavu sh.milioni 20.
Mwenyekiti wa
halmashauri hiyo, Haruna Kasele aliongeza kuwa, katika robo ya kwanza ya 2019/2020
halmashauri hiyo imetoa jumla ya sh.milioni 345 kwa vikundi 57 ambapo vikundi 28 ni
vya wanawake na vilipata sh.milioni 184, vikundi 19 vya vijana sh.milioni 133.5 na
vikundi 10 vya wenye ulemavu sh.milioni 27.5.
Alibainisha kuwa mkazo umeendelea
kuwekwa ili kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa, hadi sasa jumla ya sh.milioni 247 zimesharejeshwa
ambapo akinamama wanaongoza kwa kurejesha sh.milioni 181, vijana sh.milioni 63 na walemavu
sh.milioni mbili.
Tags
Uchumi