Juhudi za kuwasajili Traore, Havertz, Ndombele, Sessegnon, Neymar zashika kasi

Winga wa Wolves na Uhispania Adama Traore anang'ang'aniwa na Manchester City na Juventus. MANCHESTER City na Juventus zimeongeza juhudi za kumsaka winga wa Wolves na Uhispania Adama Traore, 24 ambaye pia anayatiwa na Barcelona hii ikiwa ni kwa mujibu wa ESPN. Aidha, kwa mujibu wa Goal, Chelsea wanapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Kai Havertz, 21, baada ya klabu kadhaa za Ujerumani kushindwa kufikia bei ya euro milioni 90 kumpata mchezaji huyo. Barcelona imeulizia kuhusu usajili wa kiungo wa kati wa Tottenham Mfaransa Tanguy Ndombele, 23, na mlinzi Ryan Sessegnon kutoka Uingereza katika mpango utakaohusisha ubadilishanaji wa wachezaji. (Evening Standard. Barcelona inamnyatia kiungo wa kati wa Tottenham Mfaransa Tanguy Ndombele. SPURS huenda wakamsajili kwa mkopo Sessegnon msimu huu wa joto licha ya hofu kwamba nyota ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20-inafifia chini ya ukufunzi wa Jose Mourinho. (Telegraph) Borussia Dortmund imeipatia Manchester United hadi Agosti 10 kukamilisha mchakato wa usajiliwa winga wa England Jadon Sancho, 20. (Mirror). Borussia Dortmund imeipatia Manchester United hadi Agosti 10 kumsajili winga wa England Jadon Sancho. MSHAMBULIAJI wa England Tammy Abraham, 22, ameiambia Chelsea kwamba anataka mkataba mpya wa thamani ya £130,000 kwa wiki. (Times) Mkufunzi wa West Ham David Moyes anatafakari uwezekano wa kuwanunua wachezaji wa Manchester United Phil Jones, 28, na Jesse Lingard 27. (Independent) Arsenal, West Ham na Everton wanamtaka beki wa Athletic Bilbao na Uhispania Unai Nunez,23. (AS, via Sport Witness. West Ham itafanikiwa kuwanunua Jesse Lingard na Phil Jones kutoka Man United?. RAIS wa Barcelona Josep Bartomeu amesema klabu hiyo huenda isimsajili tena mshambuliaji wa Brazil Neymar, 28,kutoka Paris St-Germain msimu huu wa joto. (RAC1 - in Spanish) Saint-Etienne ina matumaini ya kumhifadhi kwa mkopo beki wa Arsenal Mfaransa William Saliba, 19. Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar. WINGA wa Uholanzi Tahith Chong, 20, huenda akaondoka Manchester United kwa mkopo msimu ujao, kwa mujibu wa ajenti wake. (Stretty News). Barcelona imemhakikishia mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 29, kwamba yupo katika mpango wa klabu hiyo msimu ujao. (L'Equipe - in French.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news