ACT -Wazalendo, CUF, CHADEMA, SAU, NCCR-Mageuzi walipania Moshi Mjini, Buni Ramole asema akishinda mshahara wake bungeni atasamehe kusaidia maendeleo

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Buni Ramole amesema, endapo atapitishwa na tume ya taifa ya uchaguzi kugombea ubunge, na kushinda katika jimbo hilo, atatafuta wawekezaji watakaowekeza katika sekta ya viwanda na kutumia mshahara wake, kuwaletea wananchi  maendeleo, inaripoti Diramakini… 

Buni ambaye amechukua fomu kwa msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Moshi Mjini, Michael Mwandezi amekuwa mgombea wa tano, kuchukua fomu, kuomba kuteuliwa na Tume ya Taifa ya  Uchaguzi  kupeperusha bendera ya chama chake katika jimbo hilo.

Picha kwa hisani ya Mtandao.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Ramole amesema,  amechukua fomu baada ya wananchi kumuomba  na kwamba nia yake kubwa ni kuhakikisha anafufua viwanda, vitakavyochochea ukuaji wa ajira na kuwezesha mzunguko mkubwa wa fedha.

"Dhamira yangu kubwa ni kufufua viwanda Moshi, nitatafuta wawekezaji, watakaowekeza viwanda ili kuufikia uchumi wa viwanda, nitaongea zaidi kwenye majukwaa,lakini kukubwa wananchi waniamini na wanitumie vizuri katika kipindi hiki ili nikalete maendeleo,"amesema.

"Mshahara sitachukua, nitatumia akili niliyo nayo na uwezo wangu kuleta maendeleo, na nikikosa kwa sasa,itakuwa mwisho mimi kugombea,"amesema.

Buni kipindi hiki kitakuwa ni cha pili, kugombea ubunge jimbo la Moshi mjini, ambapo aligombea pia mwaka 2015, lakini hakushinda.

Msimamizi wa uchaguzi,Moshi mjini, Michael Mwandezi, amesema tayari wagombea watano wa vyama tofauti wamechukua fomu ya uteuzi katika jimbo hilo hadi kufikia leo.

Amevitaja vyama hivyo kuwa  ni Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), NCCR- Mageuzi, CUF, ACT Wazalendo.

"Hadi sasa wagombea watano  wamechukua fomu kuomba kuteUliwa na tume kugombea katika Jimbo la Moshi Mjini,"amesema Mwendezi.

Karibu! Tovuti hii ya www.diramakini.co.tz imesajiliwa rasmi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kupewa leseni namba TCRA/OCS-BL/0197/2020 chini ya Diramakini Business Limited iliyosajiliwa nchini Tanzania kwa ajili ya kukuhabarisha, kukuelimisha na kukupasha habari mbalimbali toka ndani na nje ya nchi. Je? Una habari,maulizo au tangazo, unataka kutupa ufadhili? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com Asante.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news