KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema, janga la COVID-19 limevuruga utalii duniani kote hivyo kuathiri kwa kiwango kikubwa shughuli mbalimbali za kiuchumi.
"Janga hili ni mshtuko mkubwa kwa uchumi ulioendelea, lakini kwa nchi zinazoendelea ni dharura, haswa kwa nchi nyingi ndogo za visiwani zinazoendelea na nchi za Afrika. Kwa wanawake, jamii za vijijini, watu asilia na watu wengine wengi waliotengwa kihistoria, utalii umekuwa chombo cha kuwaunganisha, kuwawezesha na kutengeneza kipato. Utalii pia ni nguzo muhimu kwa uhifadhi wa urithi,"
Akizungumza kwa njia ya video amesema, utalii ni miongoni mwa sekta muhimu zaidi duniani na sekta hiyo inatoa ajira kwa mtu mmoja katika kila watu 10 duniani huku ikitoa riziki kwa mamilioni zaidi ya watu.
Guterres amesema, sekta ya utalii inakuza uchumi na kuwezesha nchi kustawi mbali na kuwezesha watu kuendeleza utajiri wa kiutamaduni na asili na kuwaunganisha.
Tags
Kimataifa