SEKTA ya Fedha nchini Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kukuwa kwa kasi, hii ikichangiwa na mazingira wezeshi na rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje, Diramakini inakujuza kwa kina...
Mafanikio hayo ambayo yanaenda sambamba na uwekezaji wa miradi mikubwa ya kiuchumi ambayo inahitaji fedha kutoka sekta hiyo, yamewezesha kuundwa kwa benki mpya yenye nguvu kiuchumi ya Mwanga Hakika Microfinance baada ya kuungana kwa benki tatu ikiwemo Mwanga Bank, Hakika na EFC Bank.
Fuatilia mtiririko wa matukio ya uzinduzi huo katika picha hapa chini;
Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dokta Bernard Kibesse (kulia), Naibu Mwekezaji, Raymond
Tarimo pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mhandisi Ridhuan
Mringo wakifurahi baada ya kuzindua benki mpya iitwayo Mwanga Hakika
Microfinance baada ya muunganiko wa benki tatu tatu ikiwemo Mwanga
Community Bank, Hakika Microfinance Bank na EFC Tanzania Microfinance
Bank.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Jagjit Singh.
Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt.Bernard Kibesse akikata utepe kuashiria kuzindua
rasmi Benki ya Mwanga Hakika Microfinance Bank iliyotokana na muunganiko
wa benki tatu ikiwemo Mwanga Community Bank,Hakika Microfinance Bank pamoja na EFC Tanzania Microfinance Bank.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Mhandisi Ridhuan Mringo.
Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dokta Bernad Kibesse (kushoto),
Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya (katikati) wakifuatilia zoezi la
uzinduzi wa benki ya Mwanga Hakika Microfinance Ltd.Benki hiyo ni
muunganiko wa benki tatu (Mwanga Community Bank, Hakika Microfinance
Bank na EFC Tanzania Microfinance Bank).Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Mwanga Hakika Microfinance Ltd,Jagjit Singh.
Tags
Uchumi
Kuna uwekezaji nimeuona kwenye benk sijaelewa
ReplyDelete