Benki ya TPB yakabidhi madarasa, ofisi, madawati na samani mbalimbali Shule ya Msingi Kikale wilayani Kibiti

 BENKI ya TPB imekabidhi madarasa mawili, ofisi ya walimu, madawati 50 na samani za ofisi katika Shule ya Msingi Kikale iliyopo Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani. 

Mradi huo umegharamu sh.milioni 57.8 na ulikabidhiwa kwa uongozi wa shule na Mkuu wa Wilaya Kibiti,Gulamhussein Shaban Kifu aliyeambatana na viongozi mbalimbali wa Kibiti. 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi alisema benki hiyo ilianza mradi huo baada ya kupokea maombi kutoka shuleni hapo yakieleza changamoto ya majengo kwa ajili ya wanafunzi katika shule hiyo yenye wanafunzi takribani 327. 

"Tunafahamu shule hii ni kongwe sana, na kwa kipindi cha muda mrefu ilikuwa ikikabiriwa na changamoto ya madarasa,"amesema Sabasaba na kuongeza "Benki yetu ni miongoni mwa wadau wakubwa wa elimu nchini, na ni jukumu letu kusadia shule hizi zilizopo pembezoni ili nao pia wapate elimu katika mazingira bora na salama.

Mkuu wa Wilaya Kibiti Mkoa wa Pwani Gulamhussein Shaban Kifu wa pili (kulia) wakishirikiana kukata utepe na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya (TPB) Plc Sabasaba Moshingi (katikati), kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Deo Kwiyukwa, wakishirikiana uzinduzi wa madarasa mawili na madawati na ofisi za walimu katika Shule ya Msingi Kilale iliopo Ikwiriri Mkoani Pwani, anaoshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Zainabu Ndole, (kushoto) na wengine wafanyakazi wa benki hio. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Majanga (RISK), Moses Manyatta.
Kama tulivosikia awali mradi wote umegharimu Shilingi milioni 57 na laki 8, ambacho ni kiasi benki imetoa kutoka katika faida yake ambayo inapata kila mwaka."
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Kibiti,Gulamhussein Shaban Kifu ameupongeza uongozi wa benki ya TPB kwa majengo mazuri ya madarasa na ofisi katika shule ya msingi Kikale.

 "Nina amini benki hii inapokea maombi mengi sana kwa mwaka kwa ajili ya kusaidia jamii katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, ila Kikale mmekuwa miongoni kwa shule zenye bahati kwa mwaka huu kupata msaada huu kutoka TPB. 
Mkuu wa Wilaya Kibiti Mkoa wa Pwani Gulamhussein Shaban Kifu, (mbele) wakishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya (TPB) Plc Sabasaba Moshingi kukata utepe kuashiria uzinduzi wa madarasa mawili na madawati na ofisi za walimu katika Shule ya Msingi Kilale iliopo Ikwiriri Mkoani Pwani, wengine wanao shuhudia ni baadhi ya walimu na wafanyakazi wa benki hiyo .
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya (TPB) Sabasaba Moshingi wakati wa sherehe za kukabidhi madarasa mawili na ofisi za walimu, katika Shule ya Msingi Kilale Ikwiriri mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya (TPB) Sabasaba Moshingi(kulia) akifurahia jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani Mkuu wa Wilaya Kibiti Gulamhussein Shaban Kifu katika sherehe za kukabidhi madarasa mawili na ofisi za walimu, katika Shule ya Msingi Kilale Ikwiriri mkoani Pwani.

"Tunaahidi kuwa Wilaya ya Kibiti itakuwa bega kwa bega na benki hii katika kuhakikisha wananchi wa Kikale na Kibiti kwa ujumla wanapata huduma za kibenki kupitia benki hii,"amesema Kifu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news