BREAKING NEWS: BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU YAREFUSHA MUDA KWA WANAFUNZI

 “Katika mwaka wa masomo 2020/21 tumepitishiwa bajeti na Bunge shilingi Bilioni 464 ambapo tunatarajia kutoa mikopo mipya kwa wanafunzi wasiopungua 54,000 kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza; www.diramakini.co.tz


Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul- Razaq Badru ameyasema hayo muda mfupi jijini Dar es Salaam huku akibainisha kuwa, bodi hiyo imeongeza muda wa siku 10 kwa waombaji wa mkopo kuanzia Septemba Mosi hadi 10/2020.

Badru ameyasema hayo katika maonesho ya vyuo vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini humo.

Amesema kuwa, wamefikia uamuzi huobaada ya kupokea maombi kutoka kwa wadau ambao ni wazazi na waombaji mkopo kutokana na mchakato huo kutakiwa kumalizika leo usiku.

Badru amesema, mchakato wa kupokea maombi hayo ulianza Julai 21/2020 ambapo hadi leo bodi hiyo imepokea jumla ya maombi ya wanafunzi 85,921 ambapo kati ya maombi hayo 71,888 sawa na asilimia 84 yamewasilishwa kikamilifu na kuthibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).

Amesema, wapo wanafunzi wanaoendelea na kufanya jumla kuu ya wanafunzi wanaopewa mkopo kufikia 132,200 ambao watapata mikopo kupitia bajeti mpya iliyoongezeka kutoka sh. Bilioni 450 mwaka uliopita.

 

“Ni ongezeko kubwa sana na ndiyo maana tumeamua kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata mikopo, ndiyo maana serikali ipo makini katika uwekaji wa fedha zaidi,”amesema.

Amesema, uombaji wa mkopo umefikia asilimia 84 huku maombi 14,033 sawa na asilimia 16 yakiwa katika hatua mbalimbali na kutakiwa kukamilishwa na waombaji.

 “Mwaka jana tulipokea maombi 87,000 na kati ya hao maombi 82,000 sawa na asilimia 94 yalikuwa kamilifu, mwaka jana kulikuwa na changamoto ya wanafunzi kutokukamilisha kujaza sasa mwaka huu tukaamua kutoa elimu kwa wazazi, walimu namna ya utaratibu wa kuomba mkopo kuanzia Mei mwaka huu,”amesema. 

Naye Meneja Mkuu Mwendeshaji Biashara kutoka Shirika la Posta, Mwanaisha Ally Said amesema hadi leo asubuhi wanafunzi 63,768 wamehudumiwa na shirika hilo nchini nzima Bara na Visiwani katika kutuma maombi ya mkopo kwa wanafunzi.

“Wanafunzi waliokamilisha taratibu ni 71,000 ambapo kati ya hao 63,768  wameshatuma na wameingia kwenye mtandao wetu,”amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news