"Kwa mujibu wa Kifungu cha 40 (2) cha Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 pingamizi linaweza kuwekwa kwa wagombea wa ubunge kama zuio kwa mgombea aliyeteuliwa kuanzia saa 10 jioni ya siku ya uteuzi hadi saa 10 jioni ya siku inayofuatia baada ya siku ya uteuzi. Ni jambo la kushangaza kuona vipo baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vinatangaza uwepo wa wagombea waliopitishwa bila kupingwa kabla ya muda wa mapingamizi kuisha, tunawasihi sana ndugu zetu wanahabari kuepuka kutoa taarifa ambazo hazijathibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi;
MKURUGENZI WA UCHAGUZI NEC, DKT.WILSON CHARLES. |
Amesema, taarifa zinazosambaa katika mitandao mbalimbali na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa,wapo wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani waliopitishwa bila kupingwa hazina usahihi huku akiongeza kuwa, hadi sasa hakuna pingamizi lolote lililotolewa kwa wagombea wa urais wa vyama 15 ambao jana walipitishwa na tume kugombea.
Dkt.Charles amesema, haiwezekani wawepo wagombea ambao wamepita bila kupingwa wakati muda wa kuwekewa mapingamizi ambao kisheria bado uunaendelea hadi saa 10 jioni.
Tags
Siasa