TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Manyara (TAKUKURU) inamshikilia Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Ufana, Emanuel Petro Guse kwa kuendesha biashara ya mikopo umiza bila kuwa na leseni ya biashara ya ukopeshaji.
Mkuu wa TAKUKURU mkoani Manyara, Holle Makungu amesema, awali walipokea malalamiko toka kwa mwananchi eneo la Bashnetu aliyekopa kwa Mchungaji huyo kiasi cha shilingi 200,000 na kurejesha shilingi 400,000, lakini bado akawa anadaiwa shilingi 480,000 kutokana na mkopo huo wa 200,000 hali iliyotulazimisha kumuita Mchungaji Guse kwa mahojiano.
"Tulimtaka Mchungaji huyo aje kwa hiari yake katika ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Manyara, lakini alikaidi, hivyo tulilazimika kuwatuma makachero wetu kwenda kumkamata.
Makachero walipomkamata Mchungaji Guse walimuuliza iwapo anafanya biashara ya kukopesha fedha ambapo Mchungaji huyo alikana na kudai kuwa hajawahi kufanya biashara hiyo.
Makachero wa TAKUKURU walilazimika kufanya upekuzi ofisini kwa mchungaji huyo ambapo waliweza kupata mikataba ya mikopo umiza 48 nyumbani kwake,".
Baada ya kukusanya nyaraka katika upekuzi, makachero wa TAKUKURU walimchukua hadi ofisi zetu mjini Babati na kufanya naye mahojiano ambapo mtuhumiwa alikiri kufanya biashara hiyo ya mikopo umiza bila leseni.
Mtuhumiwa alipoulizwa kuhusu mlalamikaji wetu alikiri kwamba ni kweli alimkopesha shilingi 200,000, na kwamba mtuhumiwa amekwisha kurejesha kiashi cha shilingi 400,000, lakini bado ana mdai tena shilingi 480,000.
Mchungaji huyo anaendelea kushikiliwa na TAKUKURU Mkoa wa Manyara wakati tukiendelea na uchunguzi wa mikataba 48 iliyokutwa nyumbani kwake wakati wa upekuzi.
"TAKUKURU Mkoa wa Manyara inatoa wito kwa mwananchi yeyote aliyeathirika na mikopo umiza ya mchungaji huyo katika maeneo ya Bashneti Ufana, Madunga na vijiji jirani tunaomba wafike ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Manyara zilizopo Babati Mjini Jumamosi Agosti 29, 2020 ili changamoto zao ziweze kushughulikiwa kwa pamoja.
Ni rai kwa wana Manyara kutokubali kulipa riba hizo kubwa kwa wakopeshaji ambao hawana leseni na hawalipi kodi serikalini kwa kuwa biashara hizo ni haramu na kinyume cha sheria, toeni taarifa TAKUKURU wakopeshaji hao waweze kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria,"anafafanua Mkuu wa TAKUKURU mkoani Manyara, Holle Makungu, www.diramakini.co.tz

Tags
Habari