MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Semistolces Kaijage kwa mamlaka aliyopewa amemteua Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mama Samia Suluhu kuwa mgombea wa kiti cha Makamu wa Rais kupitia CCM na kukabidhiwa seti za fomu na nyaraka muhimu kuwa kumbukumbu kwao.
Hatua hiyo inefikiwa baada ya Dkt.Magufuli kurejesha fomu za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Njedengwa jijini Dodoma leo.
Rais ameongozana na Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan. Kwa habari au matangazo (diramakini@gmail.com).
Tags
Siasa