CATHERINE SAMBA-PANZA ASEMA YUPO TAYARI KURUDI IKULU

RAIS wa zamani wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza ambaye aliiongoza nchi hiyo kati ya mwaka 2014 na 2016, ametangaza kuwa, yupo tayari kuwania nafasi hiyo na kupambana jukwaani na Rais Faustin Archange Touadera kupitia Uchaguzi Mkuu ambao utafanyika Desemba 27, mwaka huu.

Aliyewahi kuwa Rais wa mpito Jamhuri ya Afrika ya Kati,Catherine Samba-Panza akiwahutubia wajumbe (hawapo pichani) kuwaelezea dhamira yake ya kurejea Ikulu ya Banjui. PICHA NA REUTERS/Antoine Rolland.

Samba-Panza ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 64, na ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kuliongoza taifa la watu milioni 4.6 katika kipindi kigumu cha migogoro ya kisiasa amesema katika hafla iliyofanyikia mjini Banjui kuwa, atachukua uamui huo baada ya watu wengi kumshawishi kufanya hivyo.

“Kutokana na ongezeko migogoro ya kisiasa na usalama hafifu kutokana na mivutano mbalimbali kutoka pande zinazokinzana, wengi wameona ninatosha na kunishawishi nigombee urais," Rais huyo mstaafu aliwaeleza wafuasi wake kupitia hotuba aliyoitoa mjini humo.

"Natangaza rasmi kwamba nitawania katika uchaguzi wa urais, ninao uwezo mkubwa kwa sababu niliiongoza nchi hii katika kipindi kigumu,"amefafanua.

Samba-Panza aliteuliwa kuwa Rais wa taifa hilo Januari 2014, ilipokuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na anatajwa kuwa anaweza kufanya vizuri katika uchaguzi huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news