TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) tayari imewateua wagombea watatu kwa ajili ya kuwania nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wagombea hao ni Dkt.John Magufuli (CCM), John Shibuda (ADA-TADEA) na Leopard Mahona (NRA). Uteuzi huo umefanywa leo jijini Dodoma na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) nchini Tanzania kupitia Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Semistocles Kaijage.
Aidha, wagombea wenza ni Samia Suluhu Hassan (CCM), Konde Kijongoo (ADA Tadea) na Ally Khamis Hassan (NRA) zaidi www.diramakini.co.tz
Tags
Siasa