CCM kumekucha, watia nia 10,000 kuchujwa, Bashiru ataja watakaoendelea

Katibu Mkuu wa CCM, Dokta Ali Bashiru akizungumza na vyombo habari wakati wa uzinduzi wa  Kituo cha CCM cha Mawasiliano ya Habari za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dokta Ali Bashiru amewataka wote waliotia nia kugombea ubunge kubaki kwenye majimbo yao kusubiri majina yatakayopitishwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho inayokaa Dodoma Agosti 20,mwaka huu, anaripoti Richard Mwaikenda kutoka Dodoma.

Dokta Bashiru amesema, inabidi wabaki kwenye majimbo yao ili iwe rahisi kwa watakaopitishwa kugombea, kwenda kuchukua fomu, kutafuta wadhamini na kurejesha fomu ili Agosti 25, mwaka huu wazirejeshe Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya uteuzi.

Ameyasema hayo leo baada ya kuzindua Kituo cha CCM cha Mawasiliano ya Habari za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania ambao kampeni zake zinatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

Amesema kuwa, leo kimekaa kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, kuandaa taarifa ya wagombea itakayopelekwa kesho katika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuchuja majina kwa mujibu wa katiba ya chama hicho na hatimaye kuyapeleka Halmashauri Kuu Agosti 20, mwaka huu itakayoteua jina moja la mgombea kwa kila jimbo na wagombea wa viti maalumu.

“Kazi ya Sekretarieti siyo kufanya uteuzi bali ni kuandaa nyaraka, kufanya uchambuzi  taarifa  za vikao vya wilaya na mikoa za watia nia ubunge na wa viti maalumu ngazi ya Taifa, tunachambua na kuandaa mapendekezo na kuvipeleka Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa  na hatimaye  Halmashauri Kuu ya Taifa kwa aijili ya uteuzi.

“Tunarajia sifa za chama chetu ndiyo msingi mkubwa, na chama chetu kwa sifa zake tutakuwa pia na viongozi wenye sifa hizo, kwa hiyo sifa za viongozi wanaotakiwa zipo kwenye Katiba na kanuni za uteuzi, mwadilifu, mchapakazi, jasiri, mzalendo, msikivu kwa anaowaongoza, mwenye nidhamu ya kutii maelekezo ya vikao wa chama,”amesema Dokta Bashiru.

Amesema kuwa, anatatarajia katika waliotia nia kugombea zaidi 10,000,  kati yao watapata wagombea bora, kwa sababu ya kipimo cha chama ni kuwa na hazina ya  viongozi, ni idadi ya waliotia nia na kwamba  mchakato umekuwa wazi kwa nchi nzima, kwenye urais, ubunge na udiwani. 

Kuhusu wawakilishi ameseutaratibu wake utafanyika baadaye kwani  ratiba ya uchaguzi na kampeni imekuwa tofauti kwa Zanzibar.


Je, una habari,maulizo au tangazo? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news