CCM yazindua Kituo cha Mawasiliano kuhusu habari za Uchaguzi Mkuu Tanzania

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dokta Ali Bashiru akiwasiliana na Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, kwa simu iliyopigwa kwenye kompyuta mpakato ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano cha CCM kuhusu Habari za Uchaguzi kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo.
Dokta Bashiru akiangalia picha za wagombea urais kupitia CCM zilizopambwa upenuni mwa kituo hicho. Wagombea hao ni Dokta John Magufuli anayewania urais wa Jamhuri ya Muungano na Mgombea Mwenza Samia Suluhu Hassan pamoja na Mgombea urais Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM, Gabriel Athuman akiangalia mpangilio ulivyo ndani ya kituo hicho.

Afisa Tehama wa CCM, Magoti Wambura akimuonesha Katibu Mkuu wa CCM, Dokta Bashiru, jinsi wanavyowasiliana na  viongozi, wanachama na umma kupitia kwenye kompyuta mpakato  wakati wa uzinduzi wa kituo hicho cha habari za uchaguzi.
Baadhi ya watumishi wa kituo hicho
Dokta Bashiru akiangalia kituo hicho wakati akipata maelezo kutoka kwa Afisa Tehama, Wambura (kushoto). Kulia ni Gabriel Athuman.
Afisa Tehama wa CCM, akitoa maelezo kwa Dk. Bashiru jinsi kituo hicho kitakavyopokea taarifa mbalimbaliza za uchaguzi kupitia kituo hicho.
Dk Bashiru akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho ambapo alisema kuwa hivi sasa kituo hicho kitakuwa kinakusanya taarifa mbalimbali za uchaguzi kutoka kwa  viongozi wa CCM, Wanachama na Umma na baada ya uchaguzi  kazi yake kubwa itakuwa kukusanya Taarifa za Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
Dokta Bashiru akizungumza na wanahabari kuhusu kazi ya kituo hicho.
Mtumishi wa kituo hicho, Debora Kiyuga akiwa tayari ameanza kazi ya mawasiliano
Neema Mfugale akiweka mambo sawa
Zuhura Hassan akiwa kazini
Baadhi ya watumishi wakiwa kazini kituoni hapo

Afisa akiendelea kutekeleza majukumu yake
 Muonekano wa kisasa wa kituo hicho. Picha zote na Richard Mwaikenda.


Je, una habari,maulizo au tangazo? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news