Corona yaondoa mshikamano wa Serikali na Kanisa, vijana watuma barua ya kukemea UN

 AGOSTI 10, mwaka huu vikundi 155 vya vijana vyenye wanachama milioni mbili kutoka nchi 62 duniani kote walituma barua kwa pamoja kwenda kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ikiwemo Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) na Ofisi ya Umoja wa Mataifa Tume Kuu ya Haki za Binadamu (OHCHR).

Barua hizo zilizoonwa na tovuti hii ya www.diramakini.co.tz zilihusisha maombi ya kukekemea na kupinga unyanyapaaji dhidi ya Kanisa la Shincheonji, dhehebu jipya lenye makao makuu yake nchini Korea Kusini na Shirika la HWPL (Heavenly Culture World Peace and Restoration of Light ) lenye ushirika na UN-ECOSOC.

Mwakilishi wa barua hiyo, Mkurugenzi na Mwanzilishi wa FREE WATCH AFGHANSTAN, Mobeenullah Aimq ameieleza www.diramakini.co.tz kuwa,anakubaliana na wasiwasi wa Umoja wa Mataifa kwenye mateso yanayowakumba vikundi vya walio wadogo na waliokuwa kwenye hatari pia uvunjwaji wa haki za binadamu unaondelea kwa visingizio vya kupambana na janga la virusi vya corona (COVID-19).

Amesema, ili kutatua tatizo hilo alipendekeza vijana duniani kote kukata rufaa kwenye jumuiya za kimataifa.

Alisisitiza kwa ufasaha zaidi kwamba, Serikali ya Korea Kusini inapaswa kuachana na mateso dhidi ya Kanisa la Shinchoenji nchini Korea Kusini.

 “Mateso dhidi ya Shincheonji na HWPL yanatakiwa kuachwa mara moja ili Serikali isiharibu sifa yao ya kimataifa, inayojulikana kama mtoaji wa amani duniani. Sifa hii inahitaji  iokolewe,”amesema Mwakilishi huyo..

Aidha, kwenye barua hizo zimeripotiwa kesi kadhaa za unyanyapaa na ukandamizaji wa Serikali ya Korea Kusini na vyombo vya habari dhidi ya mashirika hayo kwa kutoa mfano wa wasiwasi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu madhara ya uhalifu kwenye jamii, ukuaji wa chuki na kulenga makundi yaliyo kwenye hatari.

Kutokana ripoti kumekuwa na kesi 5,500 za uvunjwaji wa haki za binadamu kwa waumini wa Kanisa la Shincheonji kwa kipind hiki cha janga la Covid-19.

Katika hizo kesi kumekuwa na waumini wa kike wawili waliofariki katika mazingira ya kutatanisha. Waathirika wengi ni vijana wa kesho ambao wanapitia unyanyapaa katika sehemu za kazi na shuleni, nyumbani na kulazimishwa kulikataa dhehebu .

Pia barua inaeleza kwamba, waumini hao wa Kanisa la Shincheonji kwa bahati mbaya pia ni waathika wa janga ili la virusi vya corona. Hata kama walifuata taratibu na mwongozo wote wa Serikali katika janga husika.

 “Jambo la kushangaza zaidi ni tendo la ukamatwaji na upelelezi dhidi ya Mwenyekiti wa Kanisa la Shincheonji na Shirika la HWPL, Man Hee lee mwenye umri wa miaka 89 ambaye ukamataji wake ulidhamiriwa, pia vibali vya mashirika hayo vimebatilishwa na serikali pia mashirika hayo yamekuwa yakipitia uchunguzi mkali wa kodi. Wale wote wenye nafasi za uongozi kwenye mashirika hayo mawili wamewekwa chini ya ulinzi kwa ajiili ya uchunguzi,”imeongeza taarifa.

Gazeti la Korea Times kupitia moja ya matoleo yake limehoji kuwa, “je? Dhehebu hili ambalo sio maarufu litapata haki ?” Michael Brean, Mkurugenzi mkuu wa Insight Communications alisema, kutokana na uchunguzi unaondelea dhidi ya Kanisa la Shincheonji ni kama kitendo cha kumtafuta  mchawi ni nani? Kwani alisema Shincheonji ni sehemu sahihi kwa  wanasiasa wanaotaka kusema vibaya kanisa hilo kwa kuwa sio maarufu sana.

Katika barua hizo za ujumla zilisisitiza ukomeshwaji wa kesi za ukandamizaji dhidi ya haki za binadamu kijamii na kidini kama zinavyotokea kwa sasa nchini Korea Kusini, zinatakiwa zifike mwisho ili kuweza kupatikana kwa suluhisho ambalo ni fanisi na la umoja katika dharura hii ya leo na pia kuponywa kwa kesho.

Karibu! Tovuti hii ya www.diramakini.co.tz imesajiliwa rasmi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kupewa leseni namba TCRA/OCS-BL/0197/2020 chini ya Diramakini Business Limited iliyosajiliwa nchini Tanzania kwa ajili ya kukuhabarisha, kukuelimisha na kukupasha habari mbalimbali toka ndani na nje ya nchi. Je? Una habari,maulizo au tangazo, unataka kutupa ufadhili? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com Asante.

 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news