WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kumtanguliza Mungu mbele wakati wakijadiliana na kuteua wagombea ubunge kupitia CCM, Diramakini inakudokeza…
Rai hiyo imetolewa leo Agosti 20,mwaka huu na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Joseph Magufuli wakati akifungua kikao cha Halmashauri Kuu jijini Dodoma.
Amesema, wanachama wa chama hicho zaidi ya 10,367 walichukua fomu nafasi ya jimbo na viti maalumu huku wanachama ambao walijitokeza katika kuwania nafasi za wawakilishi ni 786.
“Pia waliojitokeza kuwania udiwani, wadi na viti maalum walikuwa 33,094, kwa maana hiyo, waliojitokeza kuwania naafasi mbalimbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi walifikia 43,461,”amewaeleza wajumbe hao.
Amesema, hatua waliyofikia iliwalazimu kufanya uchambuzi waa kina kwa sababu ya umuhimu wa nafasi hizo na kuhakikisha kila mgombea anakidhi vigezo kwa ajili ya kupeperusha bendera ya chama.“Ndugu wajumbe, ninawasihi muweke maslahi ya Taifa mbele, msichague kwa urafiki, undugu, ukanda au ukabila, tangulizeni maslahi ya Taifa mbele. Uchambuzi ulikuwa wa kina kweli kweli, tulitumia taarifa nyingi kutoka kwenye vyanzo mbalimbali na mimi nataka kuwahakikishia ndugu wajumbe nimesoma majina yote 10,367,”amesema Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa.
Karibu! Tovuti hii ya www.diramakini.co.tz imesajiliwa rasmi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kupewa leseni namba TCRA/OCS-BL/0197/2020 chini ya Diramakini Business Limited iliyosajiliwa nchini Tanzania kwa ajili ya kukuhabarisha, kukuelimisha na kukupasha habari mbalimbali toka ndani na nje ya nchi. Je? Una habari,maulizo au tangazo, unataka kutupa ufadhili? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com Asante.