MKUU wa Wilaya ya Kinondoni,Daniel Chongolo amemtaka Mkandarasi
wa Kampuni ya NAMIS CORPORATE L.T.D ambaye anajenga Soko la Tandale kuongeza kasi ya
ujenzi huo ili wafanyabiashara waweze kurudi kwenye eneo lao, inaripoti Diramakini..
Amesema, lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha inaboresha miundombinu yote ya masoko ili wafanyabiashara waweze kufanya biashara na kuendesha maisha yao na hivyo kuziwezesha halmashauri kufikia malengo hayo.
Amefafanua kuwa, mradi huo wa soko la kisasa unajengwa kwa
gharama ya sh.Bilioni 8.7, fedha ambazo zimetolewa na Serikali Kuu na kwamba tayari Mkandarasi huyo ameshalipwa fedha
zote na hivyo kusisitiza kwamba anapaswa
kufanya kazi usiku na mchana ilikukamilisha kazi yake kwa wakati.Muonekano wa soko la Tandale linaloendelea kujengwa.
“Serikali ya Rais Dokta John Magufuli imemlipa Mkandarasi pesa zote, hivyo hatudai badala yake sisi ndio tunamdai soko letu atukabidhi kwa wakati sahihi, wafanyabishara na wananchi wanasubria kwa shauku kubwa sana ukizingatia soko hili ni muhimu kwa wakazi wa Dar es Salaam, kwa sababu litahusika zaidi na biashara ya mazao ya nafaka pamoja na bidhaa nyingine,” amesema Chongolo.
Awali Meneja kutoka kampuni hiyo iliyopewa kandarasi ya
ujenzi wa soko hilo, Mhandisi James Msumari alimueleza DC Chongolo kuwa ujenzi
huo utachukua miezi 12, jambo ambalo alionesha kutokuridhishwa na muda huo na
kusema kuwa hakuna sababu ya kutumia
muda mrefu kwa kuwa fedha wanazo hivyo wanapaswa kukamilisha ujenzi kwa makubaliano
yaliyoingiwa.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Daniel Chongolo
akipata maelezo kutoka kwa Meneja mradi wa Kampuni ya ujenzi NAMIS CORPORATE
L.T.D, Mhandisi James Msumari namna ambavyo soko hilo litakavyokuwa.
Kwa upande wake, Mhandisi Msumari amesema, wamepokea maagizo na
wako tayari kuyatekeleza ili waweze kuondoa changamoto zinazowakabilio
wafanyabiashara wa eneo hilo.
Je, una habari,maulizo au tangazo? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com