DOKTA HUSSEIN MWINYI:NIMEGOMBEA NAFASI HII KWA DHAMIRA MOJA TU

 "Ndugu zangu, ninajua mna matumaini makubwa na mimi. Nataka niwahakikishieni kwamba, nimeamua kugombea nafasi hii kwa dhamira moja tu, nayo ni kuwatumikia Wazanzibari. Kwa hivyo, kuweni na matarajio, na Inshallah Mwenyezi Mungu akitujalia, kwa kushirikiana tutayatimiza;

Mgombea wa nafasi ya urais katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Hussein Mwinyi ameyasema hayo leo jijini Zanzibar muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu, www.diramakini.co.tz inakujuza zaidi...

Dkt.Mwinyi amesema, akiwa kiongozi jambo la kwanza atahakikisha anaondoa matabaka ya kila aina, matabaka ya Upemba na Uunguja, Ukusini na Kaskazini na matabaka ya dini zote ili kujenga Zanzibar mpya na kila mmoja kunufaika na maendeleo ya Zanzibar.

Pia ametoa wito kwa Wazanzibari wote kuhakikisha wanalinda amani na utulivu ili kufikia malengo ya kujenga Zanzibar mpya itakayowanufahisha wote bila kubagua mtu.

“Iwapo mtanichagua kama kiongozi wenu nitahakikisha tunajenga uchumi wa kisasa na hivyo kufikia uchumi huo vijana muwe tayari kuajiriwa popote ili kuinua uchumi wetu,”amesema Dkt.Mwinyi.

Aidha, amesisitiza kujenga miundombinu rafiki itakayoleta mazingira mazuri kwa wananchi hao ili kufikia uchumi wa kisasa na kunufaika na uchumi huo.

Wakati huo huo, Dkt.Mwinyi amesema kuwa,atahakikisha mapato yanakusanywa kwa ufasaha bila kupotea ili mapato hayo yakatekeleze miradi ya maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar.

“Hivyo basi viongozi wa chama na wanachama wote sasa ni wakati wa kuingia kazini ili kuhakikisha chama kinapata ushindi katika uchaguzi huu, kwani uchukuaji fomu ndIo kiashiria cha kipenga cha uchaguzi kupulizwa rasmi," amesisitiza Dkt.Mwinyi huku akiwahamasisha wananchi wote Oktoba 28, mwaka huu kujitokeza kwa wingi ili kutimiza haki yao.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news