Dokta Kijazi aongoza kikao cha Makamishna wote wa Jeshi la Uhifadhi Tanzania

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akiongoza kikao cha kujadili na kupitia Miundo ya Taasisi  ( organization structures ) ili kuendana na matakwa ya sheria iliyoanzisha Jeshi la Uhifadhi hapa nchini.
Kikao hicho cha juzi jijini Dodoma kilihudhuriwa na Makamishna wa Uhifadhi  wa Taasisi za Uhifadhi za Mamlaka ya Usimamizi wa  Wanyamapori Tanzania, Hifadhi za Taifa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania. Akisikiliza kwa umakini mkubwa, kushoto kwa Naibu Katibu Mkuu Dkt.Allan Kijazi, ni Mkurugenzi wa Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Maurus Msuha.Picha na WMU/Diramakini.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Kanali Martin Michael Kilugha (aliyevaa sare za JWTZ, kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi - Usimamizi wa Sheria na Mikakati ya Ulinzi na Usalama, John Nyamhanga ( kulia) wakifurahia jambo kufuatia michango ya wajumbe wa kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi na Makamishna wa Taasisi za Uhifadhi Tanzania, kilichofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. Picha na WMU/Diramakini.
 
Washiriki wa Mkutano wakifuatilia kwa umakini mkutano wa kupitia na kuhuisha Miundo ya Taasisi ili kuendana na matakwa ya sheria iliyoanzisha Jeshi la Uhifadhi. Mkutano huo ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi, umefanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.Kutoka kulia ni Kamishna wa Uhifadhi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo, Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara TANAPA, William Mwakilema na Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Huduma Saidizi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Huduma Saidizi Emmanuel Wilfred. Picha na WMU/Diramakini.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akielezea jambo wakati wa kikao chake na Makamishna wa Uhifadhi nchini, kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.Picha na WMU/Diramakini.
Washiriki wakifuatilia kwa umakini mkubwa, kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi na Makamishna wa Uhifadhi nchini, kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Picha na WMU/Diramakini.
 
Baadhi ya wakuu wa Taasisi za Uhifadhi Tanzania, wakifuatilia kwa ukaribu kikao cha kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Dkt. Allan Kijazi na Makamishna wa Uhifadhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Picha na WMU/Diramakini.
Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Dkt. Fredy Manongi, akisisitiza kuhusu utekelezaji wa sheria kwa watumishi wa Jeshi la Uhifadhi ili kuhakikisha kunakuwa na matokeo chanya katika nyanja zote. Picha na WMU/Diramakini.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi-Rasilimaliwatu, Witness Shoo ( aliyesimama ) akijibu swali lililohitaji ufafanuzi kutoka kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Kanali Martin Michael Kilugha 
(aliyevaa sare za JWTZ wa tatu kutoka kushoto kwa Witness Shoo). Picha na WMU/Diramakini.

Je, una habari,maulizo au tangazo? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news