Gavana Mike Sonko azidi kuwa shujaa Kenya, apongezwa kwa moyo upendo, unyenyekevu


GAVANA wa Jiji la Nairobi nchini Kenya, Mike Mbuvi Sonko amezidi kupongezwa ndani na nje ya Jamhuri hiyo kutokana na juhudi zake ambazo zimewezesha kurejesha faraja na matumaini kwa jamii mbalimbali.

Kwa nyakati tofauti baadhi ya raia wa Kenya waliopo ndani na nje wameielezea tovuti hii ya www.diramakini.co.tz kuwa, moja ya sifa kuu ya Gavana Mike Sonko ni pamoja na kuwa na moyo wa upendo na kujitoa kwa ajili ya wengine ambao wanapitia katika shida mbalimbali.

"Mike Mbuvi Sonko ni mchapa kazi kweli kweli,ni mtu mwenye moyo wa kujitoa kwa ajili ya wengine, Mheshimiwa Sonko, kupitia wakfu wake wa Sonko Rescue Team, amekuwa akitoa msaada wa chakula kwa familia katika vitongoji duni.

"Hatua hiyo ya kutoa vyakula na mahitaji mengine ya msingi kwa familia, imekuwa ya baraka sana, si jambo dogo, kwa kuwa si rahisi kuweza kushuhudia viongozi wengine wakiwa na moyo wa kipekee namna hii,"anasema Wanjiku katika mazungumzo na www.diramakini.co.tz 

Mbali na siasa ikiwemo ujasiriamali Gavana Sonko anatajwa kuwa ni miongoni mwa wakulima na wafugaji wa kisasa kama inavyoonekana katika picha hapa chini

 Gavana Sonko akivuna kabeji katika moja ya mashamba yake nchini Kenya.

 Gavana Sonko akiwa amenyanyua boga alilovuna katika moja ya shamba lake.

 

Gavana Sonko akiwa ameshikilia kabeji baada ya kuivuna shambani kwake.

 


 
Gavana Sonko akiwa amebeba mboga alizovuna katika moja ya mashamba yake

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news