HAWA NDIO CCM ILIOWALAZA NJE,MCHAMBUZI WA SIASA KUTOKA BEIJING ATAJA WANAKOELEKEA

“CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesajili kikosi kitamu sana,na ushindi wake unaweza kuwa mtamu sana iwapo, kila mchezaji (mteuliwa) atajielekeza katika hoja na kujipa ufahamu wa kuyaelewa mambo ambayo yanawakabili wananchi na kuwashirikisha namna ambavyo watayakabili iwapo atapata ridhaa kwao, moja ya faida kubwa ya ushindi walionayo ni pamoja na namna ambavyo Serikali iliyopo madarakani ilivyotekeleza Ilani ya Uchaguzi 2015-2020 kwa ufanisi, hivyo huu ni mwanzo mzuri kwao, na uteuzi wa leo umeonyesha dhairi kuwa CCM hii ni mpya kwelikweli,” Hayo ni maneno ya miongoni mwa wachambuzi wa masuala ya kisiasa barani Afrika aliyepo mjini Beijing, China katika mazungumzo na www.diramakini.co.tz
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt.John Magufuli (kushoto) na Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein. Viongozi hao wamekuwa msingi muhimu wa kuhakikisha majina yote zaidi ya 10,000 yanapitiwa kwa umakini hadi kupatikana wateule sahihi.

Katika mahojiano hayo, mchambuzi huyo ameueleza mtandao huu kuwa, wateule waliotangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenenzi wa CCM, Ndugu Humphrey Polepole kutoka makao makuu ya nchi jijini Dodoma, wote wanaonekana kukidhi matakwa ya wananchi katika nafasi za uwakilishi bungeni.

Amesema, pia walioachwa benchi ambao wamekaa katika nafasi za ubunge na hata serikalini kwa muda mrefu ni ishara tosha kwamba, chama hicho kimejizatiti kuondoa ile dhana ya fulani ndiye mwenye nguvu ya kukaa nafasi moja kwa muda mrefu.

Miongoni wa walioachwa benchi ni pamoja na aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, waziri na Mwenyekiti wa BUNGE ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Andrew Chenge. Raphael Chegeni (Busega),William Ngeleja (Sengerema), Peter Serukamba (Kigoma Kaskazini),Daniel Nzanzugwako (Kasulu Mjini), Charles Tizeba (Buchosa), Juma Nkamia (Chemba), 

Stephen Masele (Shinyanga Mjini),Balozi Adad Rajab (Muheza), Balozi Diodorus Kamala (Nkenge), Julius Kalanga (Monduli), Profesa Jumanne Maghembe (Mwanga), Mbaraka Bawazir (Kilosa), Suleiman Ahmed Saddiq (Mvomero), Hassan Masala (Nachingwea), Isaay Paulo (Mbulu Mjini), 

James Ole Millya (Simanjiro)Jitu Soni (Babati Vijijini),Omar Badwel (Bahi), Emmanuel Papian (Kiteto),Charles Kitwanga (Misungwi), Issa Mangungu (Mbagala), Edwin Sannda (Kondoa Mjini), Mahmound Mgimwa (Mufindi Kaskazini), Venance Mwamoto (Kilolo), Agustino Masele (Mbogwe), Godfrey Mgimwa (Kalenga).

Pia walioachwa benchi yupo, Daniel Mtuka (Manyoni Mashariki), Salum Khamis (Meatu), Prof.Tibaijuka (Muleba Kusini), Alan Kiula (Iramba Mashariki), John Kadutu (Ulyankulu), Janet Mbene (Ileje), 

Justin Monko (Singida Kaskazini),Ezekiel Maige (Msalala), Mussa Ntimizi (Igalula), Greyson Lwenge (Wanging’ombe), Dkt.Dalay Kafumu (Igunga), Mboni Mhita (Handeni Vijijini), Edward Mwalongo (Njombe Mjini), Joram Hongoli (Lupembe), Dkt.Shukuru Kawambwa (Bagamoyo), Mary Chatanda (Korogwe Mjini), Omary Kigoda (Handeni Mjini), Dkt.Haji Mponda (Malinyi).

Aidha, kuna Nimrod Mkono (Butiama), Peter Lijualikali (Kilombero), Victor Mwambalaswa (Lupa), SAUL Amon (Rungwe), Rashid Chuachua (Masasi),Jerome Bwanausu (Lulindi), Joel Mwaka (Chinolwa-Chamwino), George Lubeleje (Mpwapwa), Dkt. Mary Nagu (Hanang’), Hasna Mwilima (Kigoma Kusini), 

Kangi Lugola (Mwibara),, Oscar Mukasa (Biharamulo Magharibi), Prof. Noman Sigalla (Makete), Deogratias Ngalawa (Ludewa), Hassan Kaunje (Lindi Mjini), William Dau (Nanyumbu), Richard Mbogo (Nsimbo), Dkt.Pundenciana Kikwenmbe (Kavuu). TAARIFA ZAIDI ENDELEA KUFUAFITILA www.diramakini.co.tz

Karibu! Tovuti hii ya www.diramakini.co.tz imesajiliwa rasmi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kupewa leseni namba TCRA/OCS-BL/0197/2020 chini ya Diramakini Business Limited iliyosajiliwa nchini Tanzania kwa ajili ya kukuhabarisha, kukuelimisha na kukupasha habari mbalimbali toka ndani na nje ya nchi. Je? Una habari,maulizo au tangazo, unataka kutupa ufadhili? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com Asante.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news