ACT Wazalendo imedhamiria na imejiandaa kikamilifu kujenga na kuongoza Tanzania ya Watanzania.
Tanzania ambayo kila mtanzania; mtoto, kijana, mwanamke, mwanaume, mzee, wa kijijini na mjini ana haki sawa mbele ya sheria na ana fursa stahiki za kujenga na kujifikia ndoto zake. Tanzania ambayo, watanzania wanajivunia kuwa watanzania.
Serikali ya ACT wazalendo itahakikisha upatikani na ulinzi wa haki na ustawi wa watu wenye ulemavu, watoto hasa walioko kwenye mazingira magumu, jamii na makundi yaliyopo pembezoni na wanawake ambao ndiyo walezi wa taifa hili.
Tafiti za kisayansi zimeonyesha na kuthibitisha kuwa kuwezesha na kuwekeza kwa wanawake na makundi mengine maalumu, kuna tija endelevu kiuchumi na kijamii. Muhimu zaidi, kunaleta umoja na usawa katika jamii.Soma zaidi hapa