ILANI YA CHADEMA YA UCHAGUZI MKUU 2020-2025 HII HAPA

Ilani ya Chadema ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 hadi 2025 imetungwa kwa kuzingatia misingi ya falsafa, itikadi pamoja na madhumuni ya kuanzishwa kwa Chadema, kama ilivyofafanuliwa kwa kina katika Sura ya 3 na Sura ya 4 ya Katiba ya Chadema (Toleo la 2019).

Kwanza, Ibara 3.1.3 ya Katiba ya Chadema inaitaja falsafa ya Chadema kuwa, “Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya Nchi; na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo”.  

Pili, Ibara ya 4.1.4 ya Katiba ya Chadema inatamka madhumuni ya Chadema kuwa ni: “Kuendeleza na kudumisha Demokrasia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kujenga utamaduni wa demokrasia katika jamii kwa kutambua haki za wengi katika maamuzi; na pia kutambua haki za wachache kusikilizwa, kuheshimiwa na kulindwa, sambamba na kukubali ushindani huru, wa haki na wa wazi katika uchaguzi.” Endelea hapa


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news