Jeshi lawakamata Rais Keita, Waziri Mkuu Cisse, raia wahofia Mali

RAI nchini Mali wapo katika hali ya wasiwasi mkubwa, muda mufipi baada ya taarifa kufichuka kuwa, Rais wa Taifa hilo la Magharibi mwa Afrika, Ibrahim Boubacar Keita na Waziri Mkuu, Boubou Cisse wamekamatwa na jeshi, anaripoti Mwandishi Wetu kutoka Bamako.

Kwa sharti la kutotajwa jina lake, mmoja wa raia hao ameieleza Diramakini kutoka mjini Bamako, Mali kuwa, raia wengi wameingiwa na wasiwasi kwa hofu kuwa, huenda hali hiyo ikasababisha mauaji zaidi.

Amesema,Taifa hilo ambalo limekuwa katika maandamano ya muda mrefu ambapo raia wamekuwa wakishinikiza Rais Keita kujiuzulu kutokana na kuongezeka kwa mauaji kutoka makundi ya Kiislam nchini humo ikiwemo mdodoro mbaya wa kiuchumi, hivo kusababisha matabaka kipindi hiki mambo yanaweza kuharibika zaidi.

"Ndiyo, tuna wasiwasi mkubwa sana, bado hatujua kipi hasa kitaendelea baada ya hatua hii, lakini ni wazi kuwa, muda si mrefu wafuasi wa Keita watajibu mapigo,huu ni muda wa kumuomba Mwenyenzi Mungu atujalie heri na usalama katika Taifa letu,"amesema raia huyo mjini Bamako katika mahojiano na Diramakini.
Rais Keita ambaye alizaliwa Januari 29,1945 ni miongoni mwa wanasiasa waliodumu katika nyadhifa mbalimbali ndani ya taifa hilo kabla ya kuingia madarakani mwaka 2013. 

Viongozi walioshikiliwa na Jeshi nchini Mali. Picha na Mtandao.

Keita amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Mali kuanzia mwaka 1994 hadi 2000 na Kiongozi Mkuu wa Bunge la Mali kuanzia mwaka 2002 hadi 2007.

Pia ndiye mwanzilishi wa Chama cha Mrengo wa Kati Kushoto cha Mali (RPM) mwaka huu 2001.Raia nchini Mali wameueleza mtandao huu kuwa,hali mbaya inayojitokeza nchini humo ni kutokana na Rais huyo ambaye ilionekana kutokuwa na misimamo thabiti, kwa kuwa yeye anaegemea zaidi mrengo huo.

"Hauwezi kuamini katika jamii endelevu na Serikali endelevu kama mambo yanazidi kuharibika, ujamaa na udemokrasia ni mambo mawili tofauti, kiongozi anapaswa kuwa shupavu kwa ajili ya ustawi wa Taifa lake na watu wake, si kuendeshwa kwa maneno ya watu au makundi fulani,"anafafanua raia huyo.

Je, una habari,maulizo au tangazo? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news