SAIDI Abdallah Pandu (25) mkazi wa Taveta njia ya Uzi jijini Zanzibar anashikiliwa na polisi kwa kufanya uhalifu wa kufungua na kuiba katika nyumba ya mtu huko maeneo ya Fuoni Mambosasa Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Kijana huyo amekamatwa na doti za kanga 25, mashuka nne huku akikutwa na funguo 13 za nyumba nyingine.
Akisimulia tukio hilo,ndugu wa mwenye nyumba hiyo Zone B,Shehia ya Fuoni Mambosasa amesema,alisikia kishindo katika nyumba yao ndipo alipompigia simu dada yake na kumpa taarifa kua amesikia kishindo katika nyumba yao, ndipo dada yake akaja na kumkuta mwizi huyo na kupiga kelele za mwizi.
Amesema,hapo hapo wananchi walifika kusaidia kukamatwa kwa mwizi huyo na kufikishwa kwa Sheha ili kupelekwa Kituo cha Polisi.
Sheha wa Shehia ya Mambosasa,Asia Omari Mohamed amekiri kumpokea mwizi huyo mnamo tarehe 23 mwezi majirahuu majira ya saa kumi na nusu jioni.
Chanzo:Zanzibar24update www.diramakini.co.tz