Kondakta jela kwa kutovaa beji inayomtambulisha

KONDAKTA wa daladala, Machano Issa Khamis (25) mkazi wa Donde Unguja jijini Zanzibar amefikishwa Mahakama ya Mwanzo Mwanakwerekwe, kujibu tuhuma zinazomkabili ikiwemo kutenda kosa la kuto kuvaa beji ya utingo.


Mshitakiwa huyo akiwa utingo wa gari yenye namba za usajili Z 381 CR, inayokwenda njia namba 121, ikitokea upande wa Mtoni kuelekea Muembemakumbi alipatikana akiwa hajavaa beji ya utingo jambo ambalo ni kosa kisheria.

Aliposomewa shitaka, Mshitakiwa alilikubali na kuiomba mahakama imsamehe, ombi ambalo halikukubaliwa mahakamani hapo.

Na kutozwa adhabu ya kulipa faini ya shilingi 20,000 au kutumikia Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miezi  miwili.

Aidha, mshitakiwa Machano alifanikiwa kulipa faini hiyo ili kujinusuru kwenda Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miezi miwili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news