KUSAYA, DKT.MKINDI WAJADILI MIKAKATI KABAMBE KWA AJILI YA KILIMO CHA MBOGA, MATUNDA NCHINI

KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo,Gerald Kusaya leo amefanya kikao na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kuendeleza Mazao ya Bustani (TAHA), Dkt.Jacquline Mkindi jijini Arusha cha kujadili mikakati na mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya tasnia ya mboga mboga na matunda (horticulture) nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Gerald Kusaya (kushoto) akikabidhi ramani inayoonesha maeneo yaliyopimwa afya ya udongo kwa Mtendaji Mkuu wa TAHA, Dkt.Jacqueline Mkindi leo walipofanya mazungumzo jijini Arusha kuhusu uendelezaji wa tasni ya mboga mboga na matunda.(horticulture). PICHA NA WIZARA YA KILIMO.

Sambamba na kikao hicho, Katibu Mkuu Kusaya ameikabidhi TAHA zawadi ya ramani ya Tanzania inayoonesha viwango vya pH na afya ya udongo kwa nchi nzima na imepokelewa na Mtendaji Mkuu wa TAHA, Dkt. Jacqueline Mkindi.

Kusaya ameitaka TAHA kuendelea kuelimisha wakulima wengi zaidi kuzingatia kilimo cha kitaalam kwa kutambua aina ya udongo unaofaa kwa zao husika na mbolea gani itumike, ndio maana amekabidhi ramani hiyo kuwezesha utambuzi wa maeneo yanayofaa kwa mazao ya horticulture nchini.

“Tunaendelea kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano mkubwa na wa muda wote inaotupatia wadau wa sekta ya horticulture,"amesema Dkt.Mkindi.

Katibu Mkuu Kusaya alikuwa mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kutembelea taasisi zinazojihusisha na kilimo vikiwemo viwanda vya kuzalisha mbolea kwa matumizi ya kilimo.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news