KWA NINI ILANI YA CCM 2020-2025 IMEKUWA HIVI?

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa vyama vya TANU na ASP na baadae CCM, imejengwa katika misingi ya ujamaa na kujitegemea inayozingatia utu, usawa na haki. 

Misingi hii imeimarishwa na siasa safi na uongozi bora wa CCM na imekuwa ndio nguzo ya kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa. 

Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia viongozi waliokaa jukwaa kuu mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma juzi kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni jijini Dodoma.
CCM itaendelea kuzisimamia Serikali zake kuhakikisha kuwa zinazingatia, kulinda na kudumisha misingi hii adhimu.

CCM itahakikisha kuwa Tanzania inaendelea kulinda Uhuru wake, kudumisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, na kuimarisha Muungano wetu wenye mfumo wa serikali mbili pamoja na tunu nyingine za Taifa ikiwemo falsafa ya Mwenge wa Uhuru ili kuendelea kujenga Taifa imara linalojitegemea kiuchumi na kisiasa, lenye ustawi wa watu wake na linaloenzi na kuthamini mila nzuri, desturi na utamaduni wetu.

CCM inaamini kwamba uzalendo kwa nchi ndio msingi wa maendeleo ya kweli ya Tanzania ambayo yataletwa na Watanzania wenyewe. 

Hivyo basi, CCM itaendelea kuhimiza wananchi kuwa wazalendo kwa nchi yetu kwa kufanya kazi kwa uadilifu, bidii na maarifa kama msingi imara wa maendeleo. 

 CCM inaamini pia kuwa kila mtu ana jukumu la kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kujiletea maendeleo yake na Taifa kwa ujumla. 

Imani hii ndiyo chimbuko la kauli mbiu za Hapa Kazi Tu! na Kuacha Kufanya Kazi kwa Mazoea!  

Aidha, CCM inatambua kuwa serikali inazoziongoza zina jukumu la msingi la kuhakikisha kuwa walio wanyonge katika jamii wanapata fursa ya kipekee ya kustawisha maisha yao na kuondokana na unyonge wao ili kupunguza tofauti za matabaka. 

CCM inatambua kuwa nchi yetu ina watu wenye uwezo na rasilimali za kutosha kama vile ardhi, madini, gesi asilia, misitu, wanyama, malikale/mambo ya kale, bahari, maziwa na mito, pamoja na nafasi na fursa nzuri za kijografia. 

Rasilimali na fursa hizi zikitumiwa vizuri zitakuwa chachu kubwa kwa maendeleo ya Taifa, kama ambavyo imethibitika katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 na kwamba tukiamua tunaweza. Ni katika muktadha huu CCM inaamini kuwa Tanzania ni nchi tajiri.BONYEZA HAPA NA USOME ILANI YOTE HAPA

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news