Hatua ya leo inakuja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumchagua, Dkt. Hussein Ali Mwinyi hivi karibuni kuwa mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya chama hicho visiwani Zanzibar, ni katika Uchaguzi Mkuu unaorajiwa kufanyika Oktoba 28,mwaka huu.
Dkt.Mwinyi, ambaye ni mtoto wa rais mstaafu wa Awamu ya Pili wa nchini Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi, licha ya kuwa mwanasiasa mbobezi pia ni tabibu kitaaluma na Waziri wa Ulinzi wa sasa wa Tanzania.
Amewahi kushika nyadhifa zingine huko nyuma ikiwa ni pamoja na kuwa waziri wa afya na wa masuala ya Muungano.
Dkt.Mwinyi pia amewahi kuwa mbunge pande zote za Tanzania Bara na Visiwani.
Kwa habari au matangazo (diramakini@gmail.com)