KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet Tanzania itaipamba fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Bayern Munich na Paris Saint- Germain kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa mashabiki wa soka watakaojibu maswali mbalimbali, anaripoti Mwandishi Wetu…
Timu hizo zitakutana kwa mara ya kwanza Jumapili (Agosti
23), mwaka huu kwenye uwanja wa Estadio da Luz wa Ureno wenye uwezo wa kuingiza
watazamaji 64,642 na M-Bet imeandaa kumbi mbili, Samaki Samaki Mlimani
City na Masaki ambapo watafunga ‘screen kubwa’ kwa ajili ya
kuonyesha mpira huo.Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi.
Mushi amesema kuwa, wamefanya hivyo ili kuwakutanisha mashabiki wa soka na mbali ya kuangalia mechi, pia watajumuika pamoja na kubadilishana mawazo.
“Hii ni moja ya mikakati ya M-Bet Tanzania kuwakutanisha mashabiki pamoja na kujumuika kuangalia fainali hiyo ambapo zawadi kama za mipira, jezi, fulana na nyinginezo nyingi zitatolewa kwa wataojibu maswali ya fainali ya mechi hiyo na historia ya Ligi ya Mabingwa ya Ulaya,”amesema Mushi.
Amesema pia kutakuwa na maswali yahusiyo kampuni yao ambayo imefanikiwa kutoa washindi wengi na kuwazawadia zawadi mbalimbali ambazo zimeweza kubadili maisha yao.
Karibu! Tovuti hii ya www.diramakini.co.tz imesajiliwa rasmi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kupewa leseni namba TCRA/OCS-BL/0197/2020 chini ya Diramakini Business Limited iliyosajiliwa nchini Tanzania kwa ajili ya kukuhabarisha, kukuelimisha na kukupasha habari mbalimbali toka ndani na nje ya nchi. Je? Una habari,maulizo au tangazo, unataka kutupa ufadhili? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com Asante.