MAAFISA OFISI YA WAZIRI MKUU WAPIGWA MSASA UTEKELEZAJI MAJUKUMU




Baadhi ya maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa ufanisi na weledi. Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi hiyo na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao, jijini Dodoma tarehe 24 Agosti, 2020
Mtaalamu wa masuala ya Sera kutoka Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA),Apronius Mbilinyi akiendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu waliyokasimiwa maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mafunzo hayo ya siku tano yanajikita katika namna ya kufanya Uchambuzi wa sera, Tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sera hizo, utaalamu katika Uandishi wa Ripoti pamoja na namna bora ya  kutekeleza Uratibu.  Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri  Mkuu na kuendeshwa na Wakala hiyo jijini Dodoma tarehe 24 Agosti, 2020.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA), Dickson Mwanyika akisisitiza umuhimu wa watumishi wa umma kupata mafunzo ya kujenga uwezo kwa watumishi wa umma  lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa ufanisi na weledi. Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala hiyo, jijini Dodoma tarehe 24 Agosti, 2020.
Afisa Tawala Mwandamizi  ofisi ya Waziri Mkuu,Stephen Magoha akichangia juu ya masuala ya Uratibu wa Ofisi hiyo wakati wa mafunzo hayo.

 Maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko wakati akisisitiza umuhimu wa mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa ufanisi na weledi. Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi hiyo na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA), jijini Dodoma tarehe 24 Agosti, 2020. Picha na OWM/Diramakini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news