Maandalizi ya kibabe Ligi Kuu, usajili wafanyika juu kwa juu

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Msimbazi, leo kikosi chao kitaingia kambini na jioni kitaanza mazoezi kujiandaa na Simba Day na msimu mpya. Picha na Simba SC Tanzania.
  

MSHAMBULIAJI Chris Mugalu ambaye ni rai wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amejiunga rasmi na Simba SC ya jijini Dar es Salaam, Diramakini inakujuza zaidi...

Mugalu ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Power Dynamos ya jijini Lusaka nchini Zambia ametambulishwa rasmi Msimbazi.

Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na anaungana na washambuliaji wawili tegemeo ndani ya Simba ambao ni John Bocco na Meddie Kagere ambao msimu wa 219/20 waling'ara.

ONYANGO

Wakati huo huo, Joash Onyango raia wa Kenya amefunguka kuwa kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba SC, Francis Kahata ndiye aliyemshawishi kuja baada ya awali kuwasiliana naye.

Onyango ameongeza kwamba licha ya kuwasiliana na Kahata, pia mwenyewe alikuwa anataka kubadilisha upepo ndiyo sababu akakubali kutua Simba SC kwa ajili ya msimu ujao wa 2020/21.

Mkenya huyo mwishoni mwa wiki alisaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba SC akitokea Gor Mahia ya Kenya.

Onyango amesema kwamba alikuwa anafanya mawasiliano muda mrefu na Kahata anayecheza naye timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars na ndiye ambaye amemvuta kuja Tanzania na kutua Simba SC.

PAUL NONGA

Mbali na hayo nyota mpya wa Gwambina FC, Paul Nonga amekaririwa akisema kuwa, imemlazimu kurudisha nauli kwa Namungo ambao awali walikuwa wanahitaji aingie nao mkataba.
 
Nonga ambaye aliyekuwa Lipuli, alikuwa anahitajika kwenda kusaini mkataba Namungo kabla ya Gwambina FC ambao wamempa mkataba chini ya mwalimu Fulgence Novatus.

Amesema, awali alikuwa kwenye mazungumzo na Namungo iliyokuwa inamuhitaji, lakini karata yake imeangukia kwa Gwambina FC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news