MVUA kubwa zinazonyesha mfululizo zimeendelea kuyaathiri maeneo mengi ya Pakistan, ikiwemo mji mkuu wa kibiashara wa Karachi.
Watu wakijaribu kujiokoa katika maji ya mafuriko mjini Karachi, Pakistan. Picha na Xinhua/Rex/Shutterstock.Hali hiyo imesababisha miji kufurika maji taka ambayo yametapakaa mjini kwenda vijijini na vijijini kwenda mijini huku mamlaka zikithibitisha zaidi ya vifo 36 na uharibifu mkubwa.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo,mvua hiyo imeua watu 20 mjini Karachi na vifo 16 vimetokea Kaskazini Magharibi mwa mji wa Khyber Pakhtunkhwa baada ya kuzolewa na mafuriko.
Tags
Kimataifa