|
|
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akitangaza majina ya walioteuliwa na CCM kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu. Ungana na www.diramakini.co.tz kama inavyokupitisha hatua kwa hatua katika kila mkoa hapa chini… |
MTWARA
Polepole amesema, Jimbo la Mtwara Mjini mteuliwa ni Mtenga Hassan Selemani, Mtwara Vijijini ni Hawa Ghasia, Nanyamba ni Abdallah Chikota, Tandahimba ni Katani Katani, Newala Mjini ni George Mkuchika, Newala Vijijini ni Maimuna Mtanda, Masasi ni Geofrey Mwambe, Lulindi ni Issa Mchungahela, Ndanda ni Cecil David Mwambe, Nanyumbu ni Yahaya Ali Mhata.
ARUSHA
Arusha Mijini aliyeteuliwa kwa mujibu wa Mheshimiwa Polepole ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo.
Kwa upande wa Jimbo la Arumeru Magharibi aliyeteuliwa ni Noah Lebrus Molel, Arumeru Mashariki ni John Palangyo.
Jimbo la Karatu ni Daniel Tlemai, Longido ni Stephen Kirusya,Monduli ni Fred Lowassa, Ngorongoro ni Ole Nasha.
DAR ES SALAAM
Polepole amesema, Jimbo la Ubungo ameteuliwa Prof.Kitila Mkumbo, Jimbo la Kibamba ni Issa Jumanne Mtemvu, Kinondoni ni Abass Tarimba, Kawe ni Askofu Josephat Gwajima.
Kwa upandewa Jimbo la Kigamboni ni Dkt.Faustine Ndugulile, Jimbo la Ilala ni Mussa Zungu, Segerea ni Bonna Kamoli, Ukonga ni Jerry Slaa,Temeke ni Doroth Kilave na Mbagala ni Abdallah Chaurembo.
DODOMA
Aidha, kwa upande wa Bahi ni Keneth Nolo,Chamwino ni Deo Dejembi, Mvumi ni Livingstone Lusinde, Chemba ni Mohammed Moni, Dodoma Mjini ni Anthony Mavunde, Kongwa ni Job Ndugai, Kondoa mji ni Ally Juma Makoa, Kondoa Vijijini ni Dkt. Ashatu Kijaji.
Jimbo la Kibakwe ni George Simbachawe, Mpwapwa ni George Nataly Malima.
GEITA
Kwa upande wa Busanda ni Tumaini Magesa, Geita Mjini ni Consatantine Kanyasu, Geita Vijijini ni Joseph Kasheku (Musukuma), Bukombe ni Dotto Biteko, Chato ni Medard Kalemani, Mbogwe ni Nicodemas Maganga, Nyang'alwe ni Hussein Amar.
IRINGA
Jimbo la Iringa Mjini ni Jesca Msavatambangu, Kalenga ni Jackson Kiswaga, Isimani ni William Lukuvi, Kilolo ni Lazaro Nyamoga, Mafinga mji ni Cosato Chumi, Mufindi Kaskazini ni Exaud Kigahe, Mufindi Kusini ni David Kihenzile
KAGERA
Mheshimiwa Polepole amesemaa kuwa, kwa upande wa Bukoba Mjini aliyeteuliwa ni Stephen Byabato, Bukoba Vijijini ni Jackson Rweikiza, Nkenge ni Frolent Kyombo, Karagwe ni Innocent Bashungwa, Kyerwa ni Innocent Bilakwate, Ngara ni Ndaisaba Luhoro, Bihalamuro ni Ezra Chiwelesa, Muleba Kaskazini ni Charles Mwijage, Muleba Kusini ni Oscar Kikoyo.
KATAVI
Aidha, Polepole amesema kwa upande wa Jimbo la Mlele ameteuliwa Isack Kamwele, Kavuu Geophrei Mizengo Pinda, Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi, Nsimbo ni Anna Lupembe, Mpanda Vijijini ni Moshi Kakoso.
KIGOMA
Jimbo la Kasulu Mjini ameteuliwa Prof.Joyce Ndalichako, Manyovu ni Dkt. Philip Mpango, Buyungu ni Aloyce Kamamba, Muhambwe-Atashasta Nditiye, Kigoma Mjini ni Kirumbe Shabani Ng'enda, Kigoma Kaskazini ni Asa Nelson Makanika, Kigoma Kusini ni Nashon William, Kasulu Vijijini ni Augustine Hole.
KILIMANJARO
Kwa upande wa Jimbo la Vunjo ameteuliwa Dkt. Charles Kimei, Siha ni Dkt. Godwin Mollel, Moshi Vijijini ni Prof.Patrick Ndakidemi, Hai ni Salasisha Mafue, Same Mashariki ni Anne Kilango Malecela, Same Magharibi ni Dkt. Mathayo David Mathayo, Rombo ni Prof.Adolf Mkenda, Moshi Mjini ni Priscus Tarimo, Mwanga ni Anania Tadayo.
LINDI
Jimbo la Kilwa Kaskazini ni Ndulane Franscis, Kilwa Kusini ni Kasinge Mohammed Ally, Liwale ni Zuberi Kuchauka, Lindi Mjini ni Hamida Mohammed Abdallah, Mchinga ni Salma Kikwete, Mtama ni Nape Nnauye, Nachingwea ni Amandus Julius Chinguiye, Ruangwa ni Kassim Majaliwa.
MANYARA
Kwa upande wa Jimbo la Babati Mijini ameteuliwa Paulina Gekul, Babati Vijijini, Daniel Silo, Hanang’ ni Samwel Kadai, Mbulu Mjni ni Isai Paulo, Mbulu Vijijini ni Flatei Gregory.Jimbo la Kiteto ni Edward Kisau, Simanjiro ni Christopher Ole Sendeka.
MARA
Aidha, Jimbo la Musoma Mjini kwa mujibu wa Polepole aliyeteuliwa ni Vedastus Manyinyi, Musoma Vijijini ni Prof. Sospeter Muhongo, Bunda Mjini ni Robert Chacha Maboto, Bunda Vijijini ni Boniface Getere, Mwibara ni Charles Kajege, Butiama ni Jumanne Sagini, Rory ani Jaffary Wambura Chege, Tarime Mjini ni Mwita Michael Kembaki, Tarime Vijijini ni Mwita Waitara, Serengeti ni Dkt. Jeresabi Mkimi.
MBEYA
Kwa upande wa Jimbo la Busekelo, Polepole amesema mteuliwa ni Atupele Mwakibete, Kyela ni Ally Jumbe, Lupa ni Masache Kasaka, Mbalali ni Franscis Mtega, Mbeya Mjini ni Dkt.Tulia Akson, Mbeya Vijijini ni Oran Njeza, Rungwe ni Anthony Mwantona.
MOROGORO
Kwa upande wa Jimbo la Mlimba mteuliwa ni Godwin Kunambi, Kilombero ni Abubakar Asenga, Morogoro Mjini ni Abdul Aziz Abood, Gairo ni Ahmed Shabiby, Malinyi ni Antipas Mgungusi, Morogoro Kusini ni Innocent Kalogeres, Morogoro Mashariki ni Hamis Shaaban Taletale.
Jimbo la Mvomero ni Jonas Vanzilad, Mikumi ni Deniss Lazaro Londo, Kilos ani Prof. Palamaganda Kabudi, Ulanga ni Salim Hasham.
MWANZA
Katika Jimbo la Ukerewe aliyeteuliwa ni Joseph Mkundi, Ilemela ni Dkt. Angelina Mabula, Sengerema ni Tabasamu Hamis Mwagao, Buchosa ni Erick Shigongo James, Nyamagana ni Stanslaus Mabula, Misungwi ni Alexander Mnyeti, Sumve ni Kasalali Emmanuel Mageni, Kwimba ni Shanif Mansour, Magu ni Bonaventura Kiswaga.UNGANA NASI KILA DAKIKA KWA MATOKEO ZAIDI KUPITIA www.diramakini.co.tz
Karibu! Tovuti hii ya www.diramakini.co.tz imesajiliwa rasmi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kupewa leseni namba TCRA/OCS-BL/0197/2020 chini ya Diramakini Business Limited iliyosajiliwa nchini Tanzania kwa ajili ya kukuhabarisha, kukuelimisha na kukupasha habari mbalimbali toka ndani na nje ya nchi. Je? Una habari,maulizo au tangazo, unataka kutupa ufadhili? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com Asante.