Makamu wa Rais ateta na ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu,Tume yawapa angalizo wanasiasa

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan  ameipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kazi nzuri inayofanywa kwa kuweza kutatua changamoto mbalimbali za wananchi na kuweza kupata haki zao pale wanapodhulumiwa.

Amesema hayo alipokutana na Ujumbe wa Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora uliyoongozwa na Mwenyekiti wa wake, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu walipomtembelea kwenye makazi yake Kilimani jijini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu aliyeongoza Ujumbe wa Makamishna wa tume hiyo leo wakati ujumbe huo ulipomtembelea Makamu wa Rais kwenye Makazi yake Kilimaji jijini Dodoma.

Makamu wa Rais ameipongeza tume hiyo kwa kuweza kubadilika na kufanya kazi vizuri pamoja na kutenda haki kwa wananchi na taasisi zote kwa ujumla.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Msaafu, Mathew Mwaimu ameipongeza Serikali kwa kuweza kuwaletea wananchi maendeleo bora na kuitakia kila la heri katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.


Jaji Mwaimu amesema kuwa,tume yake haipendezewi na vitendo vya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ambao wamekuwa wakisema watu badala ya kunadi Sera za vyama vyao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news