Makamu wa Rais Samia Suluhu aongoza matembezi ya Marathon Benki ya CRDB

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiongoza matembezi ya  kilomita tano kwa ajili ya kuchangia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto katika Taasisi ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam leo. Matembezi hayo yameandaliwa na Benki ya CRDB pamoja na mbio za nusu Marathon. kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dokta Jakaya Kikwete, kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela. 

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan akisalimana na mtoto Jadian Simon Senga (6) mkazi wa Dar es salaam kabla ya kuanza kwa matembezi ya kilomita tano kwa ajili ya kuchangia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto katika Taasisi ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam leo.Matembezi hayo yameandaliwa na Banki ya CRDB pamoja na mbio za nusu Marathon.  

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni mia mbili kwa ajili ya kuchangia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto katika Taasisi ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Taasisi ya Upasusuaji  ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohammed Janabi,  kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Abdulmajid Nsekela.   

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akikamilisha kuongoza matembezi ya  kilomita tano kwa ajili ya kuchangia  gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto katika Taasisi ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam leo.Matembezi hayo yameandaliwa na Benki ya CRDB pamoja na mbio za nusu Marathon. Kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dokta Jakaya Kikwete, kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Abdulmajid Nsekela.  



Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news