JESHI la Polisi nchini Israel limeanza uchunguzi maalum dhidi ya genge la wahalifu ambalo linatuhumiwa kujihusisha na matukio ya ubakaji kwa watoto na watu wazima mjini Eilat nchini humo, Inaripoti www.diramakini.co.tz endelea…
Taswira ya mji wa Eilat nchini Israel ambao unadaiwa kukithiri matukio ya ubakaji na unyanyasaji mabinti kingono. Picha na Ofer Vaknin/haaretz/Diramakini. |
Uchunguzi huo unafanyika ikiwa ni wiki moja tu imepita tangu binti wa miaka 16 ,wahalifu hao kumfanyia ukatili wa kingono katika moja ya hoteli mjini humo.
Pia Mahakama ya Hakimu Mkazi Ashkelom jana ilisogeza siku ya kusikilizwa kesi ya mmoja wa watuhumiwa kwa siku tano zaidi, ikiwa ni moja ya hatua ya kujiridhisha kabla ya hukumu, huku mtuhumiwa mwingine akishikiliwa muda huo.
Aidha, Jeshi la Polisi limesema halitaweka wazi orodha ya watuhumiwa wa matukio hayo kwa kuwa bado uchunguzi unaendelea, ingawa mawakili wa watendewa uovu huo wamesema, watuhumiwa wanakadiriwa kufikia zaidi ya 30.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameelezea kusikitishwa na vitendo hivyo vya ubakaji, huku akisisitiza kuwa, wote wanaojihusisha na unyanyasaji huo watawajibishwa kwa wakati.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.Picha Newyork Post/Diramakini. |
“Tumesoma asubuhi ya leo, mke wangu Sarah na Mimi, kuhusu matukio ya ubakaji mjini Eilat kama ilivyochapishwa. Mshituko huu, hakuna neno zaidi, si uhalifu kwa mabinti bali ni ukatili dhidi ya utu wa binadamu,na tunayalaani kwa nguvu zote, na kwa hili lazima washukiwa wote wawajibishwe,” amesema Waziri Mkuu Benamin Netanyahu kama alivyokaririwa na www.diramakini.co.tz
Karibu! Tovuti hii ya www.diramakini.co.tz imesajiliwa rasmi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kupewa leseni namba TCRA/OCS-BL/0197/2020 chini ya Diramakini Business Limited iliyosajiliwa nchini Tanzania kwa ajili ya kukuhabarisha, kukuelimisha na kukupasha habari mbalimbali toka ndani na nje ya nchi. Je? Una habari,maulizo au tangazo, unataka kutupa ufadhili? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com Asante.