MAZUNGUMZO YA TANZANIA, UBELGIJI YAFANA, MIKAKATI KABAMBE YA MAENDELEO YARIDHIWA



Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali, Wilbert A. Ibuge akizungumza na Balozi wa Ubelgiji hapa nchini,Peter van Acker. Mazungumzo hayo ambayo yalifanyika kwa njia ya mtandao yalijikita kwenye kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji. Katika mazungumzo hayo, Balozi Ibuge aliishukuru Serikali ya Ubelgiji kupitia kwa Balozi huyo kwa ushirikiano mkubwa iliyoonesha kwa Tanzania katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19 na ushirikiano katika miradi mbalimbali ikiwemo ya sekta ya maji, kwenye baadhi ya mikoa hapa nchini. Mazungumzo hayo yalifanyika leo tarehe 28 Agosti 2020 huku Balozi Ibuge akiwa jijini Dodoma na Balozi Peter van Acker akiwa jijini Dar es Salaam .

Balozi Ibuge akimsikiliza Balozi Peter van Acker wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika kwa njia ya mtandao.

Balozi Ibuge akiwa na ujumbe aliofutana nao wakati wa mazungumzo kati yake na Balozi wa Ubelgiji hapa nchini,Peter van Acker (hayupo pichani). Kulia ni Hangi Mgaka, Katibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Anthony Mtafya, Afisa Mambo ya Nje kikao kikiendelea

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news