MHANDISI MASAUNI:NIMERIDHIKA NA MCHAKATO, ASANTENI SANA

WAGOMBEA ubunge na uwakilishi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mjini,Unguja wameelezea kuridhika na zoezi la uchukuaji fomu na urejeshaji kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa upande wa Zanzibar (ZEC).

Hayo waliyaeleza kwa nyakati tofauti, baada ya zoezi hilo kumalizika katika ofisi ya wilaya ambapo walisema wamepata ushirikiano mkubwa ndani ya ZEC.
Miongoni mwao ni Mhandisi Hamadi Yussuf Masauni anayegombea Jimbo la Kikwajuni, Ali Hassan Omar (Kingi) Jimbo la Jang’ombe, Ahmada Yahya Abdul-wakil Jimbo la Kwahani na Mohamed Suleiman Omar Jimbo la Malindi.

Masauni amesema, zoezi la upatikanaji wa wadhamini katika zoezi hilo, limekwenda vizuri na kuahidi kuwatumikia wananchi wa Kikwajuni, kwani wameonesha mwanga na mapenzi ya kumuamini katika utendaji wa kazi zake.

“Mimi ubunge wa jimbo hili sikuanza leo, ni kipindi changu cha tatu kugombea jimbo hili, hivyo,ni imani yangu kufanya mazuri zaidi ya niliyoyafanya kwa jimbo langu," amesema.

Naye mgombea wa Jimbo la Jang’ombe, Ali Hassan Omar amesema kuwa, anawashukuru  wananchi kwa umoja wao na kuwahaidi kuwa akishinda nafasi hiyo atawatumikia kwa bidii ili kuharakisha maendeleo.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news