MKE wa Rais mstaafu wa 44 nchini Marekani, Barack Hussein Obama, Michelle Obama amesema utawala wa Rais wa 45 nchini Marekani, Donald Trump umeshindwa kabisa kukidhi matakwa ya watu wa kawaida nchini humo, hivyo anamuona Joseph Robinette Biden Jr (Joe Biden) ndiye mtu sahihi kwa sasa kuiongoza Marekani, inaripoti Diramakini...
Obama ameyasema hayo katika majadiliano ya kwanza ya usiku ambayo yalikuwa ni mjadala wa kitaifa wa Chama cha Democratic kupitia mitandao kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini humo.
Amesema, Wamarekani wanahitaji kiongozi ambaye anaweza kuwa suluhisho kwa wale wote ambao wanapambana na hali ngumu ya kiuchumi na kuwa faraja kwa waliopoteza ndugu zao wakati huu wa janga la virusi vya Corona (Covid-19).
Mke wa Rais mstaafu wa 44 nchini Marekani, Barack Hussein Obama, Michelle akizungumza katika mjadala wa usiku wa kuamkia leo. Picha na DNC via AP. |
"Biden, ambaye pia amepoteza wapendwa wake na mtu ambaye anajua nini kinachowakabili wale ambao wanakaa meza tupu bila chakula, anaweza kutoa suluhisho.Naye Bernie Sanders ametumua fursa hiyo kuwashukuru mamilioni ya Wamarekani ambao waliunga mkono kampeni zake.
"Trump si Rais sahihi kwa Taifa letu. Alikuwa na muda mwingi wa kuthibitisha kuhusu upatikanaji wa ajira, hajaweza kufanya lolote, hawezi kutekeleza...hivyo ndivyo ilivyo, hivyo kama utachukua japo neno moja kutoka kwangu usiku wa leo. Kama haufikirii kuwa mambo yatazidi kuwa mabaya,niamini mimi, yatakuwa mabaya, kama tutashindwa kufanya mabadiliko katika uchaguzi huu. Tunapaswa kumchagua Joe Biden kwa kuwa maisha yetu yanategemea sana uchaguzi huu,"amefafanua Obama katika majadiliano ya usiku wa leo.
"Nawashukuruni sana, vuguvugu letu linaendelea na tunaendelea kuwa imara kila siku...lakini kama Donald Trump atachaguliwa tena, juhudi zetu zitakuwa si kitu. Trump anaiongoza Marekani kidhaifu mno,huu uchaguzi ndiyo njia sahihi ya kuandika historia katika hii nchi. Tunamuhitaji Joe Biden kuwa Rais ajaye,"amesema Sanders.
Je, una habari,maulizo au tangazo? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com
Tags
Kimataifa