LEO katika hii safu mpya ya Anatoka na Nani na Anaingia Nani tunakuletea baadhi ya tetesi zinazovuma kwa sasa katika anga la michezo, www.diramakini.co.tz
Kwa mujibu wa RAC1, Klabu ya Barcelona inatarajiwa kukatiza mkataba na Luis Suarez (33) ambaye ni mshambuliaji wa Uruguay.
Wakati huo huo, kwa mujibu wa Yorkshire Evening Post,LEEDS United wanamtaka mshambuliaji wa Argentina, Nicolas Gonzalez (22).
Hii ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Michezo wa Stuttgart, Sven Mislintat.
Nayo Klabu ya Everton kwa mujibu wa Daily Express wameridhiana na Napoli kulipa pauni milioni 31.5 ili kumpata kiungo wao wa kati, Mbrazil Allan Marques Loureiro (29).
Aidha, Tuttosport imeripoti kuwa,mshambuliaji wa Italia, Moise Kean (20), anakaribia kukamilisha mchakato wa kurudi katika klabu yake ya zamani ya Juventus kwa mkopo.
Nayo Sky sports imebainisha kuwa, Klabu ya Wolves wamepiga hatua katika mazungumzo yao na Arsenal kuhusu mkataba wa miaka minne wa beki wa Uingereza, Ainsley Maitland-Niles (22).