MKURANGA YATAMBULISHA MRADI WA STENDI YA KISASA KWA WADAU SEKTA YA USAFIRISHAJI

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani imekutana na wadau mbalimbali wa sekta ya usafirishaji na kutambulisha mradi wa stendi mpya ya kisasa itakayojengwa katika Kijiji cha Kipara mpakani Mkuranga mkoani hapa, anaripoti MWANDISHI WETU.

Kikao hicho awali kilifunguliwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mhandisi Mshamu Munde, ambaye ni Peter Nambunga ambaye alielezea mradi huo na umuhimu wake hasa katika lengo kuu la kukuza uchumi wa nchi na upatikanaji wa ajira kwa watu wa rika na elimu mbalimbali.

“Kikao cha leo ni kikao chenye tija sana kwa huu mradi tunaotarajia kuuanza, hivyo wadau na washirki wa kikao tunaomba sote kwa pamoja tutoe mawazo ambayo yatapelekea kufanya mradi wetu uwe wenye sura nzuri na ya kuvutia, lakini pia uwe mradi ambao utaleta mafanikio na kuongeza chachu ya maendeleo katika halmashauri yetu na nchi kwa ujumla,"amesema.
 
Nao wadau wa sekta ya usafirishaji walioshiriki katika kikao hicho wametoa maoni yao tofauti namna ya kufanikisha mpango huo ambao utakua chachu ya mafanikio na maendeleo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.
 
Delphina Mathias mwakilishi kutoka DART amesema, kwa kushirikia na TANROAD wameandaa awamu ya sita ya mradi huo ambayo itaanzia Mbagala na kuishia eneo linalotarajiwa kujengwa stendi ya kisasa, aliongeza kwa kusema hali hiyo itapelekea wilaya kuongeza mapato, lakini pia mji kukua na hii itapelekea kitengo cha mipango miji kuupanga mji kwa kasi kuendena na kasi ya maendeleo inatyotarajiwa.
Mdau mwingine ambaye pia nia Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mkuranga,Safina Msemo amesisitza kwa kusema kuwa uwepo wa ofisi ya maendeeo ya jamii katika eneo la stendi ni muhimu sana hii itapelekea jamii itakayofanya kazi katika eneno hilo kujifunza mambo mbalimbali ya kijamii, lakini itakua chachu ya kutatua baadhi ya changamoto zitakazowakumba watumiaji wa stendi hiyo.
 
Sambamba na hilo, Said Shamte ambaye ni kiongozi kutoka katka Chama cha Umoja wa Wasafirishaji wa Abiria Kusini mwa Tanzania (UWASAKUTA) alisisitiza kuwa, wapo tayari kushrikiana na Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya kwa kuelekeza magari yote na malori ya mizigo kuanza kulitumia eneo lile mapema watakapoanza kuruhu kutumika.
 
Nae John Bukoli mtaalamu wa mradi huo alielezea mpangilio wa mradi unavyotakiwa kufanyika, na amesisitiza kuwatumia watalaamu kutoka sekta mbalimbali ikiwemo wataalamu wa mazingira, wabunifu wa majengo na wakadiria majengo pamoja na wote ambao watashirikishwa kwa lengo moja a kutengeza stendi yenye kukidhi mahitaji yote na yenye ubora wa viwango vya juu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, Mhandisi Mshamu Munde alimalizia kwa kusema hekari 50 zimetolewa na Serikali kwa kumega Msitu wa Hifadhi ya Vikindu na kubwa zaidi mradi huo utatekelezwa kwa kutumia vyanzo vya fedha za ndani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news