NA DIRAMAKINI
KAANAELI Akyoo (50) ambaye ni mkazi Kisimiri Chini wilayani Arumeru,Arusha amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akikabiliwa na tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya mkoani humo.
Picha na Getty Images.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na upande wa Jamhuri mbele ya Hakimu Mushi imedai kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 19, mwaka 2020 huko katika Kijiji cha Kisimiri Chini wilayani humo.
Inadaiwa kuwa, siku ya tukio mshtakiwa Akyoo alikutwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa kilog 160 huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa na kinyume cha sheria.
Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande hadi Septemba 7, mwaka huu kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
Aidha, kwa mujibu wa upande wa Jamhuri upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.
Tags
Mahakamani